-
Wale Wanaotembea Katika Nuru HushangiliaMnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
-
-
2 Tunapozingatia hilo, tunaweza kuelewa uzito wa hali inayofafanuliwa na nabii Isaya. Alisema hivi: “Tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu.” (Isaya 60:2) Ni wazi kwamba giza hilo si giza halisi. Isaya hakumaanisha kwamba siku fulani jua, mwezi, na nyota zitaacha kuangaza. (Zaburi 89:36, 37; 136:7-9) Badala yake, alikuwa akizungumzia giza la kiroho. Lakini giza la kiroho laweza kusababisha kifo. Hatuwezi kuishi bila nuru ya kiroho kwa muda mrefu kama vile tusivyoweza kuishi bila nuru halisi.—Luka 1:79.
3. Kwa kuzingatia maneno ya Isaya, Wakristo wapaswa kufanya nini?
3 Kwa kuzingatia hilo, ni jambo muhimu kutambua kwamba ijapokuwa maneno ya Isaya yalitimizwa katika Yuda la kale, yanatimizwa kwa kiwango kikubwa zaidi leo. Naam, katika wakati wetu ulimwengu umefunikwa na giza la kiroho. Katika hali hiyo hatari, nuru ya kiroho ni muhimu kuliko mambo yote.
-
-
Wale Wanaotembea Katika Nuru HushangiliaMnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
-
-
4. Maneno ya kiunabii ya Isaya yalitimizwa lini mara ya kwanza, lakini tayari kulikuwa na hali gani katika siku zake?
4 Maneno ya Isaya kuhusu jinsi ambavyo giza lingeifunika dunia yalitimizwa mara ya kwanza Yuda lilipofanywa ukiwa na watu wake walipokuwa katika utekwa Babiloni.
-