-
Je, Utakuwepo Katika Ulimwengu Mpya?Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 15
-
-
6. Unabii wa nne unaotaja “mbingu mpya na dunia mpya” watabiri nini?
6 Sasa na tuchunguze usemi unaosalia wa “mbingu mpya na dunia mpya,” kwenye Isaya 66:22-24: “Kama vile mbingu mpya na nchi [“dunia,”NW] mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA. Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.”
7. Kwa nini tufikie mkataa wa kwamba andiko la Isaya 66:22-24 litatimizwa wakati ujao?
7 Unabii huo ulitimizwa miongoni mwa Wayahudi waliorudishwa katika nchi yao, lakini kungekuwa na utimizo mwingine. Lazima utimizo huo ungetokea baadaye sana, baada ya barua ya pili ya Petro na Ufunuo kuandikwa, kwa kuwa barua hizo zataja ‘mbingu na dunia mpya’ za wakati ujao. Twaweza kutarajia utimizo huo mkubwa na ulio kamili katika mfumo mpya.
-
-
Je, Utakuwepo Katika Ulimwengu Mpya?Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 15
-
-
10. Kwa nini unaweza kuwa na hakika kwamba ulimwengu mpya hautaharibiwa daima na waovu?
10 Isaya 66:24 latuhakikishia kwamba amani na uadilifu za dunia mpya hazitakuwa hatarini kamwe. Waovu hawataiharibu dunia kamwe. Kumbuka kwamba andiko la 2 Petro 3:7 lasema kwamba tunangojea “siku ya hukumu na ya uangamizo wa watu wasiomwogopa Mungu.” Watakaoharibiwa ni watu wasiomwogopa Mungu. Hakuna madhara yatakayowapata wasio na hatia, tofauti na vile itukiavyo mara nyingi katika vita vya wanadamu, ambapo majeruhi walio raia huwa wengi kuliko askari. Hakimu Mkuu atuhakikishia kwamba siku yake itakuwa ya kuangamiza watu wasiomwogopa Mungu.
11. Isaya anaonyesha ni nini kitampata yeyote anayekataa Mungu na ibada yake?
11 Waokokaji waadilifu wataona kwamba neno la Mungu la kiunabii ni la kweli. Mstari wa 24 hutabiri kwamba ‘mizoga ya watu waliomwasi’ Yehova itakuwa uthibitisho wa hukumu yake. Huenda maneno ya waziwazi ambayo Isaya alitumia yakawa yenye kushtua. Hata hivyo, yanapatana na jambo hakika la kihistoria. Nje ya kuta za Yerusalemu la kale kulikuweko mahali mbalimbali pa kutupa takataka na, pindi kwa pindi, mizoga ya wahalifu walioonekana kuwa hawastahili mazishi ya heshima.a Huko funza na moto mkali zingemaliza upesi takataka hizo na mizoga hiyo. Kwa wazi, mfano wa Isaya waonyesha mfano wa hukumu ya Yehova dhidi ya waasi ambayo haiwezi kubadilishwa.
-