-
Ole Wao Waasi!Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Watainama chini ya wafungwa tu, wataanguka chini yao waliouawa.” (Isaya 10:3, 4a)
-
-
Ole Wao Waasi!Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Baadhi yao watakuwa wafungwa wa vita, “watainama chini,” au kuchutama, kati ya wafungwa wengine, ilhali wengine nao watauawa, na maiti za waliokufa vitani zitafunika maiti zao. “Utukufu” wao watia ndani mali yao waliyopata kwa ufisadi, itakayoporwa na adui.
21. Kwa kuzingatia adhabu ambazo Israeli imepata, je, hasira ya Yehova juu yao imekoma?
21 Isaya amalizia ubeti huu wa mwisho kwa onyo lenye kuhofisha: “Pamoja na hayo yote [ole zote ambazo zimelipata taifa hilo kufikia sasa] hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.” (Isaya 10:4b) Naam, Yehova angali na mengi ya kuambia Israeli. Mkono wa Yehova ulionyoshwa hautarudishwa nyuma hata atoapo pigo la mwisho na lenye kuangamiza kwa ufalme wa kaskazini ulioasi.
-