-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Katika Isaya 44:6, NW, kwa kufaa Yehova anakieleza cheo chake kuwa ndiye Mungu mweza yote mmoja tu na wa pekee, akisema: “Mimi ndiye wa kwanza na wa mwisho, na mbali na mimi hakuna Mungu.”a Yesu anapojitokeza mwenyewe kwa mtajo wa cheo “wa Kwanza na wa Mwisho,” yeye hadai kuwa yu sawa na Yehova, yule Muumba Mtukufu. Yeye anatumia mtajo wa cheo aliopewa kwa kufaa na Mungu. Katika Isaya, Yehova alikuwa akitoa taarifa kuhusu cheo Chake kisicho na kifani akiwa ndiye Mungu wa kweli. Yeye ni Mungu milele, na mbali na yeye hakuna Mungu kweli kweli. (1 Timotheo 1:17)
-
-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
a Katika Kiebrania cha awali kwenye Isaya 44:6, hakuna neno dhihirisho pamoja na maneno “wa kwanza” na “wa mwisho,” hali katika elezeo la Yesu kuhusu yeye binafsi katika Kigiriki cha awali kwenye Ufunuo 1:17, linapatikana lile neno dhihirisho. Kwa hiyo, kisarufi, Ufunuo 1:17 huonyesha mtajo wa cheo, hali Isaya 44:6 huelezea Uungu wa Yehova.
-