-
“Msiwatumainie Wakuu”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
13. Ni mambo gani yanayomngoja Yesu kule mbele, lakini anaonyeshaje kuwa ana moyo mkuu?
13 Mwana mzaliwa pekee wa Yehova ananyanyaswa na baadhi ya wale wanaomkataa, na jambo hilo pia limetabiriwa: “Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.” (Isaya 50:6) Kulingana na unabii, Mesiya atateswa na kuaibishwa na wapinzani wake. Yesu anajua ataaibishwa. Na anajua atanyanyaswa hivyo kwa kadiri gani. Hata hivyo, wakati wake duniani unapokaribia kumalizika, haonyeshi hofu. Anapiga moyo konde akiwa mgumu kama gumegume na kwenda Yerusalemu, ambako uhai wake wa kibinadamu utakoma. Huko njiani, Yesu anawaambia wanafunzi wake hivi: “Sisi hapa, tunasonga mbele kupanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa binadamu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu, na waandishi, nao watamhukumu adhabu ya kifo na watamkabidhi kwa watu wa mataifa, nao watamfanyia ucheshi na watamtemea mate na kumpiga mijeledi na kumuua, lakini siku tatu baadaye atafufuliwa.” (Marko 10:33, 34) Dhuluma yote hiyo itachochewa na makuhani wakuu na waandishi, wanaume ambao kulingana na kiwango cha ujuzi wao wanapaswa kutambua kwamba haifai kutenda hivyo.
14, 15. Maneno ya Isaya kwamba Yesu angepigwa na kuaibishwa yanatimizwaje?
14 Usiku wa Nisani 14, 33 W.K., Yesu yumo katika bustani ya Gethsemane pamoja na baadhi ya wafuasi wake. Anasali. Ghafula, kundi la wafanya-ghasia linatokea na kumpeleka kizuizini. Lakini yeye haogopi. Anajua Yehova yu pamoja naye. Yesu anawahakikishia mitume wake waliojawa na hofu kuwa kama angalitaka angaliweza kumsihi Baba yake apeleke malejioni zaidi ya 12 ya malaika ili kumwokoa, lakini anaongezea hivi: “Katika kisa hicho, Maandiko yangetimizwaje?”—Mathayo 26:36, 47, 53, 54.
15 Kila jambo lililotabiriwa kuhusu majaribu na kifo cha Mesiya linatimia. Baada ya kesi iliyoundwa kilaghai kufanyika mbele ya Sanhedrini, Yesu anahojiwa na Pontio Pilato, naye anaagiza Yesu apigwe viboko. Askari Waroma ‘wanampiga kichwani kwa tete na kumtemea mate.’ Hivyo maneno ya Isaya yanatimizwa. (Marko 14:65; 15:19; Mathayo 26:67, 68) Ingawa Biblia haitaji kwamba baadhi ya ndevu za Yesu zinang’olewa—hiyo ikiwa ni ishara ya madharau mengi—hakuna shaka kwamba inatukia hivyo, sawa na vile Isaya alivyotabiri.c—Nehemia 13:25.
-
-
“Msiwatumainie Wakuu”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
c Inafaa kuangalia kwamba, katika Septuagint, Isaya 50:6 inasema hivi: “Niliutoa mgongo wangu upigwe mijeledi, na mashavu yangu yapate mapigo.”
-