-
Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Baada ya kutaja juu ya kupata mamlaka kwa zile falme nne zilizotokana na milki ya Aleksanda, malaika Gabrieli asema hivi: “Wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama.
-
-
Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
17. (a) Uingereza ilikuwa na uhusiano gani na Milki ya Roma? (b) Milki ya Uingereza yahusianaje na ufalme wa Makedonia na Ugiriki?
17 Kwa hiyo, basi, historia yamtambulisha yule “mfalme mwenye uso mkali” na mwenye ujeuri kuwa nani? Uingereza ilichipuka upande wa kaskazini-magharibi kutoka katika Milki ya Roma. Kufikia mwanzoni mwa karne ya tano W.K., kulikuwa na mikoa ya Roma mahali ilipo Uingereza ya sasa. Hatimaye, Milki ya Roma ikadidimia, lakini ustaarabu wa Ugiriki na Roma uliendelea kuwa na uvutano katika Uingereza na katika sehemu nyingine za Ulaya zilizokuwa chini ya milki ya Roma. “Milki ya Roma ilipoanguka, Kanisa lilichukua mahali pake,” akaandika mshindi wa Tuzo la Nobeli Octavio Paz, mshairi aliyekuwa pia mwandishi huko Mexico. Aliongezea kusema hivi: “Wakuu wa Kanisa, na pia wasomi wa baadaye, waliingiza falsafa za Kigiriki katika fundisho la Kikristo.” Na mwanafalsafa aliye pia mwana-hisabati wa karne ya 20, Bertrand Russell alionelea hivi: “Ustaarabu wa Magharibi, uliotokana na Ugiriki, wategemea desturi za kifalsafa na kisayansi zilizoanzia Mileto [jiji la Kigiriki katika Asia Ndogo] miaka elfu mbili na nusu iliyopita.” Kwa hiyo, tungeweza kusema kwamba utamaduni wa Milki ya Uingereza ulitokana na ufalme wa Makedonia na Ugiriki.
18. Ile pembe ndogo iliyopata kuwa “mfalme mwenye uso mkali” katika “wakati wa mwisho” ni nini? Fafanua.
18 Kufikia mwaka wa 1763 Milki ya Uingereza ilikuwa imeshinda washindani wake wenye nguvu, Hispania na Ufaransa. Tangu wakati huo na kuendelea milki hiyo ilijidhihirisha kuwa mtawala wa bahari na pia serikali ya ulimwengu ya saba ya unabii wa Biblia. Hata baada ya zile koloni 13 za Amerika kujitenga na Uingereza mwaka wa 1776 na kuwa Marekani, Milki ya Uingereza ilipanuka na kufikia robo ya uso wa dunia na robo ya wakazi wa dunia. Serikali ya ulimwengu ya saba ilizidi kupata nguvu wakati ambapo Marekani ilishirikiana na Uingereza ili kufanyiza serikali ya ulimwengu ya Uingereza na Marekani. Kiuchumi na kijeshi, kwa kweli serikali hiyo ilikuwa imepata kuwa “mfalme mwenye uso mkali.” Kwa hiyo, ile pembe ndogo iliyokuwa kali kisiasa katika “wakati wa mwisho” ni Serikali ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani.
-