-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
29, 30. (a)“Silaha za kusini” zilishindwaje kukabiliana na shambulio kutoka kaskazini? (b) Mfalme wa kaskazini alipataje ‘kusimama katika nchi ya uzuri’?
29 Malaika wa Yehova alitabiri hivi zaidi: “Mfalme wa kaskazini atakuja, na kufanya kilima [“atauzingira,” BHN], na kuupiga mji wenye maboma; na silaha za kusini hazitaweza kumpinga, wala watu wake wateule, wala hapatakuwa na nguvu za kumpinga.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
30 Majeshi ya Ptolemy wa Tano, au “silaha za kusini,” yalishindwa na shambulio kutoka kaskazini. Huko Paneas (Kaisaria Filipi), Antiochus wa Tatu alimfukuza Jenerali Scopas wa Misri pamoja na watu 10,000 aliochagua, au ‘wateule wake,’ hadi Sidoni, “mji wenye maboma.” Huko Antiochus wa Tatu ‘aliuzingira,’ na kuiteka bandari hiyo ya Foinike mwaka wa 198 K.W.K.
-