-
Aokolewa Asiliwe na Simba!Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Kwa hiyo, wakataja jambo hilo moja kwa moja, wakisema: “Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.”a—Danieli 6:6, 7.
8. (a) Kwa nini Dario angeona sheria iliyopendekezwa kuwa yenye kupendeza? (b) Mawaziri na maliwali walikusudia nini hasa?
8 Rekodi za kihistoria zathibitisha kwamba lilikuwa jambo la kawaida kwa wafalme wa Mesopotamia kuonwa na kuabudiwa kama miungu. Kwa hiyo, bila shaka Dario alipendezwa na pendekezo hilo. Pia huenda jambo hilo lilionekana kuwa lenye faida. Kumbuka kwamba Dario alikuwa mgeni kwa watu waliokuwa wakiishi Babiloni. Sheria hiyo mpya ingemwimarisha akiwa mfalme, nayo ingechochea halaiki za watu waliokuwa wakiishi Babiloni wawe waaminifu na kuunga mkono serikali hiyo mpya. Ingawa hivyo, mawaziri na maliwali hawakupendezwa na hali nzuri ya mfalme walipokuwa wakipendekeza amri hiyo. Kusudi lao la kweli lilikuwa kumnasa Danieli, kwa kuwa walijua kwamba ilikuwa desturi yake kusali kwa Mungu mara tatu kwa siku kwenye madirisha yaliyo wazi katika chumba chake cha paa.
9. Kwa nini sheria hiyo mpya haingewatatiza watu wengi wasio Wayahudi?
9 Je, kizuizi hicho cha sala kingetatiza jumuiya zote za kidini za Babiloni? Sivyo, hasa kwa kuwa katazo hilo lingedumu mwezi mmoja tu. Isitoshe, ni watu wachache sana wasio Wayahudi ambao wangeona kuabudu mwanadamu kwa muda kuwa kuridhiana. Msomi mmoja wa Biblia ataarifu hivi: “Kumwabudu mfalme kulikuwa kawaida kwa mataifa hayo yenye kuabudu sanamu sana; na kwa hiyo Wababiloni walipoagizwa wamwabudu mshindi—Dario Mmedi—kama mungu, walikubali mara moja kufanya hivyo. Wayahudi peke yao ndio walioudhika na dai hilo.”
-
-
Aokolewa Asiliwe na Simba!Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
a Kuwepo kwa “tundu la simba” huko Babiloni kwathibitishwa na ushuhuda wa maandishi ya kale yanayoonyesha kwamba watawala wa nchi za Mashariki walifuga wanyama wa pori katika bustani zao.
-