-
Tutatembea Katika Jina la Yehova Milele!Mnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 15
-
-
15. Unaweza kuelezaje kwa maneno yako mwenyewe unabii wa Mika 4:1-4?
15 Tunapofikiria unabii huo, tunaona kwamba sasa Mika anatoa ujumbe wa tumaini wenye kusisimua. Tunapata maneno yenye kutia moyo kama nini katika Mika 4:1-4!
-
-
Tutatembea Katika Jina la Yehova Milele!Mnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 15
-
-
Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha BWANA wa majeshi kimesema hivi.”
-
-
Tutatembea Katika Jina la Yehova Milele!Mnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 15
-
-
Kwa kuwa wamefua panga zao kuwa majembe, hata leo watu hao wanaishi kwa amani pamoja na Mashahidi wenzao na watu wengine. Inafurahisha kama nini kuwa kati yao!
Kuazimia Kutembea Katika Jina la Yehova
18. ‘Kuketi chini ya mzabibu na mtini wako’ humaanisha nini?
18 Tunasisimuka kuona wengi wakijifunza njia za Yehova wakati huu ambapo watu duniani pote wanaogopa sana. Tunatamani sana wakati ambapo hivi karibuni watu wote wanaompenda Mungu hawatajifunza vita tena bali wataketi chini ya mzabibu na mtini wao. Mara nyingi mitini hupandwa katika mashamba ya mizabibu. (Luka 13:6) Kuketi chini ya mzabibu na mtini wako humaanisha kuwa na amani, ufanisi, na usalama. Hata sasa, uhusiano wetu pamoja na Yehova hutupatia amani ya akili na usalama wa kiroho. Hali hizo zitakapokuwako chini ya utawala wa Ufalme, hatutaogopa chochote, tutakuwa salama salimini.
-