-
Yehova Huchukia Mwenendo wa HilaMnara wa Mlinzi—2002 | Mei 1
-
-
Kufunga Ndoa na Mtu Asiyeamini
13, 14. Ni mwenendo gani wa hila ambao Malaki alielekezea fikira?
13 Kuanzia mstari wa 10 na kuendelea, Malaki sura ya 2 yaelekezea fikira hila kwa njia iliyo wazi zaidi. Malaki akazia mienendo miwili inayohusiana, naye atumia neno “hila” mara kadhaa. Ona kwamba Malaki alianza kutoa shauri lake kwa kuuliza maswali haya: “Je! sisi sote hatuna baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana [“hila,” NW], tukilinajisi agano la baba zetu?”
-
-
Yehova Huchukia Mwenendo wa HilaMnara wa Mlinzi—2002 | Mei 1
-
-
Muktadha unatusaidia kufahamu sababu iliyofanya jambo hilo liwe baya sana. Mstari wa 10 unasema kwamba walikuwa na baba mmoja tu. Baba huyo si Yakobo (aliyepewa jina Israeli), wala si Abrahamu, wala Adamu. Andiko la Malaki 1:6 linaonyesha kwamba ‘baba huyo mmoja tu’ ni Yehova. Taifa la Israeli lilikuwa na uhusiano pamoja na Mungu, nao walihusishwa katika agano alilofanya na baba zao. Mojawapo ya sheria katika agano hilo inasema: “Usioane nao, binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake.”—Kumbukumbu la Torati 7:3.
-