-
Kila Mtu Ataketi Chini ya Mtini WakeMnara wa Mlinzi—2003 | Mei 15
-
-
Yesu alitumia tena mfano wa mtini ili kuonyesha hali mbaya ya kiroho ya taifa hilo. Alipokuwa akisafiri kutoka Bethania kwenda Yerusalemu, siku nne kabla ya kifo chake, aliona mtini uliokuwa na majani mengi lakini haukuwa na matunda yoyote. Kwa kuwa tini za mapema hutokea wakati mmoja na majani—nyakati nyingine hata kabla ya majani kutokea—mti huo haukuwa na faida yoyote kwa sababu haukuwa na matunda.—Marko 11:13, 14.b
Kama vile mtini usiozaa ulivyoonekana kuwa unasitawi, taifa la Wayahudi lilionekana tofauti na lilivyokuwa. Lakini taifa hilo halikuwa limezaa matunda yanayompendeza Mungu, na hatimaye likamkataa Mwana wa Yehova mwenyewe. Yesu aliulaani mtini huo usiozaa, na siku iliyofuata wanafunzi wake wakaona kwamba ulikuwa umenyauka. Mti huo uliokauka ulifananisha ifaavyo jinsi ambavyo Mungu angekuja kuwakataa Wayahudi waliokuwa watu wake wateule.—Marko 11:20, 21.
-
-
Kila Mtu Ataketi Chini ya Mtini WakeMnara wa Mlinzi—2003 | Mei 15
-
-
b Kisa hiki kilitukia karibu na kijiji cha Bethfage. Jina la kijiji hicho linamaanisha “Nyumba ya Tini za Mapema.” Huenda jambo hilo likaonyesha kwamba kijiji hicho kilikuwa maarufu kwa mavuno mazuri ya tini za mapema.
-