-
Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
-
-
4. (a) Paulo alikuwa na fungu gani katika kazi ya Kikristo ya kujenga? (b) Kwa nini yaweza kusemwa kwamba Yesu na pia wasikilizaji wake walijua umuhimu wa misingi ifaayo?
4 Ikiwa jengo litakuwa imara na lenye kudumu, lahitaji msingi ufaao. Hivyo, Paulo aliandika: “Kulingana na fadhili isiyostahiliwa ya Mungu niliyopewa, kama mwelekezi wa kazi za ufundi mwenye hekima niliweka msingi.” (1 Wakorintho 3:10) Akitumia kielezi sawa na hicho, Yesu Kristo alisimulia juu ya nyumba iliyookoka dhoruba kwa sababu mjenzi wake alikuwa amechagua msingi imara. (Luka 6:47-49) Yesu alijua yote kuhusu umuhimu wa misingi. Alikuwepo Yehova alipoweka msingi wa dunia.a (Mithali 8:29-31) Waliomsikiliza Yesu pia walithamini misingi ifaayo. Nyumba zenye misingi ifaayo pekee ndizo zingeweza kuokoka mafuriko ya ghafula na matetemeko ya dunia ambayo nyakati nyingine yalitokea huko Palestina.
-
-
Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
-
-
7. Tunaweza kujifunza nini kutokana na kujirejezea kwa Paulo kuwa “mwelekezi wa kazi za ufundi mwenye hekima”?
7 Paulo alitaja kwamba alifundisha hivyo “kama mwelekezi wa kazi za ufundi mwenye hekima.” Taarifa hiyo haikuwa ya kujisifu. Ilikuwa tu ya kukiri zawadi ya ajabu ambayo Yehova alikuwa amempa—ile ya kupanga na kuelekeza kazi. (1 Wakorintho 12:28) Ni kweli kwamba, leo sisi hatuna zawadi za kimuujiza walizopewa Wakristo wa karne ya kwanza. Nasi huenda tusijione kuwa walimu wenye kipawa. Lakini kwa namna fulani yenye maana, sisi ni wenye kipawa. Ebu fikiria: Yehova hutupa roho yake takatifu itusaidie. (Linganisha Luka 12:11, 12.) Nasi twampenda Yehova na tunao ujuzi wa mafundisho ya msingi ya Neno lake. Kwa kweli hizo ni zawadi za ajabu tuwezazo kutumia kufundisha wengine. Acheni tuazimie kuzitumia ili kuweka msingi ufaao.
-