-
Kushiriki Faraja Ambayo Yehova HuandaaMnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
-
-
Dhiki ya Paulo Katika Asia
13, 14. (a) Paulo alifafanuaje wakati wa dhiki kali aliyojionea Asia? (b) Huenda ikawa Paulo alikuwa akifikiria kisa kipi?
13 Aina ya mateso ambayo kutaniko la Korintho lilikuwa limepatwa nayo kufikia wakati huo haingeweza kulinganishwa na zile dhiki nyingi ambazo Paulo alilazimika kuvumilia. Hivyo, aliweza kuwakumbusha hivi: “Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi. Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu awafufuaye wafu, aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa.”—2 Wakorintho 1:8-10.
14 Wasomi fulani wa Biblia huamini kwamba Paulo alikuwa akirejezea ghasia katika Efeso, ambayo ingewagharimu Paulo na pia waandamani wake wawili Wamakedonia waliosafiri naye, Gayo na Aristarko, uhai wao. Wakristo hao wawili waliingizwa kwa nguvu mahali pa michezo palipokuwa pamejaa kikundi cha wafanya-ghasia ‘waliopiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa kama saa mbili, wakisema, Artemi [mungu wa kike] wa Waefeso ni mkuu.’ Hatimaye, ofisa wa jiji alifaulu kuunyamazisha umati. Tisho hilo kwa uhai wa Gayo na Aristarko lazima liwe lilimtaabisha sana Paulo. Kwa hakika, alitaka kuingia na kusababu na hicho kikundi cha wafanya-ghasia chenye ushupavu, lakini alizuiwa asihatarishe uhai wake katika njia hiyo.—Matendo 19:26-41.
15. Ni hali ipi ya kupita kiasi ambayo huenda ikafafanuliwa kwenye 1 Wakorintho 15:32?
15 Hata hivyo, huenda ikawa Paulo alikuwa akifafanua hali mbaya zaidi kuliko tukio hilo ambalo limetangulia. Katika barua yake ya kwanza kwa Wakorintho, Paulo aliuliza hivi: “Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani?” (1 Wakorintho 15:32) Huenda hilo likamaanisha kwamba uhai wa Paulo ulihatarishwa na watu walio kama hayawani na pia wanyama-mwitu halisi katika stediamu ya Efeso. Nyakati nyingine wahalifu waliadhibiwa kwa kulazimishwa kupigana na hayawani-mwitu huku umati wenye tamaa ya kumwaga damu ukitazama. Ikiwa Paulo alimaanisha kwamba alikuwa amekabili hayawani-mwitu halisi, lazima awe alihifadhiwa kimuujiza katika dakika ya mwisho ili asife kifo chenye jeuri, kama vile Danieli alivyookolewa kutoka katika vinywa vya simba halisi.—Danieli 6:22.
-
-
Kushiriki Faraja Ambayo Yehova HuandaaMnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
-
-
16. (a) Kwa nini wengi wa Mashahidi wa Yehova waweza kufananisha hali zao na dhiki zilizompata Paulo? (b) Twaweza kuwa na uhakika gani kuhusu wale waliokufa kwa sababu ya imani yao? (c) Kuponea kifo chupuchupu kwa Wakristo fulani kumekuwa na matokeo gani mazuri?
16 Wakristo wengi wa siku ya kisasa waweza kuhusianisha hali zao na dhiki zilizompata Paulo. (2 Wakorintho 11:23-27) Leo, pia, Wakristo ‘wamelemewa mno kuliko nguvu zao,’ na wengi wamekabili hali ambamo ‘wamekata tamaa ya kuishi.’ (2 Wakorintho 1:8) Watu kadhaa wamekufa mikononi mwa wauaji wa kimakusudi wa watu wengi na wanyanyasaji wakatili. Twaweza kuwa na uhakika kwamba uwezo wa Mungu wenye kufariji uliwawezesha kuvumilia na kwamba walikufa, mioyo na akili zikiwa zimekazwa kikiki kwenye utimizo wa tumaini lao, liwe la kimbingu au la kidunia. (1 Wakorintho 10:13; Wafilipi 4:13; Ufunuo 2:10) Katika visa vingine, Yehova ameelekeza mambo, na ndugu zetu wameokolewa kutoka kifo. Hakuna shaka kwamba wale ambao wamepitia wokovu huo wamekuza tumaini lililoongezeka “katika Mungu, awafufuaye wafu.” (2 Wakorintho 1:9) Baadaye, waliweza kusema wakiwa na usadikisho mkubwa hata zaidi walipokuwa wakishiriki pamoja na wengine ujumbe wenye kufariji wa Mungu.—Mathayo 24:14.
-