-
Utii Je, Ni Somo Muhimu Utotoni?Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 1
-
-
“Ili Ipate Kuwa Vema Kwako”
Paulo alionyesha manufaa nyingine ya utii alipoandika: “‘Heshimu baba yako na mama yako’; ambayo ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi: ‘Ili ipate kuwa vema kwako nawe upate kudumu muda mrefu juu ya dunia.’” (Waefeso 6:2, 3; Kutoka 20:12) Ni katika njia zipi ambazo kutii wazazi hufanya hali ya mtu iwe njema?
Kwanza, si kweli kwamba wazazi wana umri mkubwa na uzoefu mwingi kuliko sisi? Ingawa huenda wasijue mengi kuhusu kompyuta au masomo mengine yanayofundishwa shuleni, wazazi wanajua mengi kuhusu maisha na jinsi ya kukabiliana na matatizo ya maisha. Kwa upande mwingine, vijana hawafikiri kwa njia yenye usawaziko nao hufanya hivyo kwa sababu ya kukosa ukomavu. Hivyo, wao hupata madhara kwa kufanya maamuzi harakaharaka, mara nyingi kwa sababu ya msongo wenye kudhuru wa marika. Kwa kufaa, Biblia yasema: “Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto.” Suluhisho ni nini? “Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.”—Mithali 22:15.
Utii hauleti manufaa tu katika uhusiano wa mzazi na mtoto. Ili jamii ya wanadamu iweze kutenda vizuri na kwa matokeo, lazima kuwe na ushirikiano, ambao pia wataka kiasi fulani cha utii. Kwa mfano, amani, upatano, na furaha katika ndoa hutokana na kuwa tayari kufikiria haki na hisia za yule mwingine wala si kutokana na kuwa mwenye kudai mno. Ili biashara au kazi yoyote ifanikiwe ni lazima waajiriwa wajitiishe kazini. Kutii sheria na kanuni za serikali huepusha mtu na adhabu na vilevile humletea angalau kadiri fulani ya usalama na ulinzi.—Waroma 13:1-7; Waefeso 5:21-25; 6:5-8.
Mara nyingi vijana wasiotii mamlaka wanakuwa watu wasiofaa katika jamii. Kinyume cha hilo, utii ambao mtu hujifunza utotoni waweza kumnufaisha katika maisha yake yote. Inafaa kama nini kujifunza utii tangu utotoni!
-
-
Utii Je, Ni Somo Muhimu Utotoni?Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 1
-
-
Kumbuka kwamba kama mtume Paulo alivyosema, amri ya kutii wazazi ina ahadi mbili, yaani, ili “ipate kuwa vema kwako nawe upate kudumu muda mrefu juu ya dunia.” (Italiki ni zetu.) Uthibitisho wa kutimizwa kwa ahadi hiyo wapatikana kwenye Mithali 3:1, 2: “Mwanangu, usiisahau sheria yangu, bali moyo wako uzishike amri, zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.” Uhusiano wa kibinafsi pamoja na Yehova sasa na uhai udumuo milele katika ulimwengu mpya wenye amani ndio manufaa kubwa ambayo wale wanaotii watapata.—Ufunuo 21:3, 4.
-