-
Kutia Muhuri Israeli wa MunguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Zile Pepo Nne
3. (a) Ni utumishi gani wa pekee unaofanywa na malaika anaouona Yohana? (b) Ni nini kinachofananishwa na “pepo nne”?
3 Kabla ya Yehova kuachilia kiruu hiki, malaika wa kimbingu wanafanya utumishi wa pekee. Sasa Yohana anaona hilo katika njozi: “Baada ya hili mimi niliona malaika wanne wakisimama juu ya kona nne za dunia, wakishika sana pepo nne za dunia, kwamba upepo wowote usipate kupuliza juu ya dunia au juu ya bahari au juu ya mti wowote.” (Ufunuo 7:1, NW) Hili linamaanisha nini kwa sisi leo? Hizi “pepo nne” ni ufananisho halisi wa hukumu yenye kuharibu inayokaribia kuachiliwa juu ya jamii mbovu ya kidunia, juu ya “bahari” yenye kusukasuka ya binadamu waasi-sheria, na juu ya watawala walioinuka mfano wa miti ambao wanapata uungaji-mkono na utegemezo kutoka kwa watu wa dunia.—Isaya 57:20; Zaburi 37:35, 36.
4. (a) Malaika wanne wanawakilisha nini? (b) Tokeo linakuwa nini juu ya tengenezo la kidunia la Shetani wakati pepo nne zinapoachiliwa?
4 Hapana shaka, hawa malaika wanne wanawakilisha vikundi vinne vya kimalaika, ambavyo Yehova anatumia kuzuia utekelezo wa hukumu yake mpaka wakati uliowekwa. Malaika hao waachiliapo pepo nne za hasira-kisasi zizunguke vuruvuru wakati ule ule mmoja kutoka kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi, kumbo hilo litakuwa kubwa mno. Litafanana, lakini kwa kadiri kubwa mno, na utumiaji wa Yehova wa pepo nne kutawanya Waelamu, akiwavunjavunja na kuwaulia mbali kabisa. (Yeremia 49:36-38) Itakuwa dhoruba ya upepo mkubwa mno yenye kukumba zaidi ya ile “tufani” ambayo kwayo Yehova alifutilia mbali taifa la Amoni. (Amosi 1:13-15, NW) Hakuna sehemu ya tengenezo la Shetani duniani ambayo itaweza kusimama katika siku ya kiruu cha Yehova, wakati yeye anapotetea enzi kuu yake kwa umilele wote utakaokuja.—Zaburi 83:15, 18; Isaya 29:5, 6.
5. Unabii wa Yeremia unatusaidiaje kuelewa kwamba hukumu za Mungu zitaenea dunia yote nzima?
5 Je! sisi tunaweza kuwa na hakika kwamba hukumu za Yehova zitakumba dunia nzima? Sikiliza tena nabii wake Yeremia: “Tazama! Afa moja linaenda kutoka taifa moja kwenda kwenye jingine, na tufani kubwa yenyewe itaamshwa juu kutoka sehemu za mbali zaidi sana za dunia. Na wale wenye kuuawa na Yehova kwa hakika watakuja kuwa katika siku hiyo kutoka mwisho mmoja wa dunia hadi kufika mwisho mwingine kabisa wa dunia.” (Yeremia 25:32, 33, NW) Ni wakati wa dhoruba hii yenye tufani kwamba giza litagharikisha ulimwengu huu. Mawakili wao wenye kutawala watatikiswa waingie ndani ya utowesho. (Ufunuo 6:12-14) Lakini wakati ujao hautakuwa wenye giza kwa kila mmoja. Basi, ni kwa ajili ya nani zile pepo nne zinazuiwa?
Kuwatia Muhuri Watumwa wa Mungu
6. Ni nani anayeambia malaika wazuie pepo nne, na hilo linaruhusu wakati kwa ajili ya nini?
6 Yohana anaendelea kueleza jinsi baadhi ya watu wanavyotiwa alama kwa ajili ya kuokoka, akisema: “Na mimi nikaona malaika mwingine akipanda juu kutoka kwenye zukio la jua, akiwa na muhuri wa Mungu anayeishi; na yeye alilia kwa sauti kubwa kwa wale malaika wanne ambao kwao ruhusa ilipewa ya kudhuru dunia na bahari, akisema: ‘Msidhuru dunia au bahari au miti, mpaka baada ya sisi tuwe tumetia muhuri watumwa wa Mungu wetu katika vipaji vya nyuso zao.’”—Ufunuo 7:2, 3, NW.
7. Ni nani hasa aliye malaika wa tano, na ni ithibati gani inayotusaidia tuthibitishe utambulisho wake?
7 Ingawa huyu malaika wa tano hatajwi jina, ithibati yote inaonyesha kwamba lazima awe Bwana Yesu aliyetukuzwa. Kupatana na kuwa kwa Yesu Malaika Mkuu, yeye anaonyeshwa hapa akiwa na mamlaka juu ya wale malaika wengine. (1 Wathesalonike 4:16; Yuda 9) Yeye anapanda juu kutoka mashariki, kama “wafalme kutoka zukio la jua”—Yehova na Kristo wake—ambao wanakuja kutekeleza hukumu, kama walivyofanya wafalme Dario na Sairasi wakati waliponyenyekeza Babuloni wa kale. (Ufunuo 16:12; Isaya 45:1; Yeremia 51:11; Danieli 5:31, NW) Malaika huyu anashabihi Yesu katika njia ya kwamba yeye ameaminishwa kazi ya kutia muhuri Wakristo wapakwa-mafuta. (Waefeso 1:13, 14) Na zaidi, wakati pepo zinapoachiliwa, ni Yesu anayeongoza majeshi ya kimbingu katika kutekeleza hukumu juu ya mataifa. (Ufunuo 19:11-16) Basi, kimantiki, Yesu angekuwa ndiye wa kuamuru kwamba uharibifu kwa tengenezo la kidunia la Shetani uzuiwe mpaka watumwa wa Mungu wawe wametiwa muhuri.
-
-
Kutia Muhuri Israeli wa MunguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Picha ya ukurasa mzima katika ukurasa wa 114]
-