-
Ufalme wa Mungu Ni Bora Katika Njia ZoteMnara wa Mlinzi—2006 | Julai 15
-
-
Yesu hatatawala akiwa peke yake. Kuna wengine watakaotawala pamoja naye wakiwa wafalme na makuhani. (Ufunuo 5:9, 10; 20:6) Mtume Yohana aliandika hivi kuwahusu: “Nikaona, na, tazama! Mwana-Kondoo amesimama juu ya Mlima Sayuni, na pamoja naye 144,000 . . . ambao wamenunuliwa kutoka duniani.”—Ufunuo 14:1-3.
Mwana-Kondoo ni Yesu Kristo akiwa Mfalme aliyetawazwa wa Ufalme wa Mungu. (Yohana 1:29; Ufunuo 22:3) Mlima Sayuni unarejelea mbinguni.a (Waebrania 12:22) Yesu pamoja na washirika wenzake 144,000 wanatawala wakiwa mbinguni. Hapo ni mahali penye utukufu kama nini! Wakiwa mbinguni, wanaona mambo mengi. Kwa kuwa kiti cha ufalme huo kiko mbinguni, “ufalme wa Mungu” huitwa pia “ufalme wa mbinguni.” (Luka 8:10; Mathayo 13:11) Hakuna silaha zozote, hata za nyuklia, zinazoweza kuifikia na kuiharibu serikali hiyo ya mbinguni. Haiwezi kushindwa, nayo itatimiza kusudi la Yehova.—Waebrania 12:28.
-
-
Ufalme wa Mungu Ni Bora Katika Njia ZoteMnara wa Mlinzi—2006 | Julai 15
-
-
a Mfalme Daudi wa Israeli la kale aliiteka ngome ya Mlima Sayuni wa kidunia kutoka kwa Wayebusi na kuifanya kuwa jiji lake kuu. (2 Samweli 5:6, 7, 9) Pia, alilipeleka Sanduku takatifu huko. (2 Samweli 6:17) Kwa kuwa Sanduku lilihusianishwa na kuwapo kwa Yehova, Sayuni liliitwa mahali pa makao ya Mungu, nalo linafaa kabisa kuwakilisha mbinguni.—Kutoka 25:22; Mambo ya Walawi 16:2; Zaburi 9:11; Ufunuo 11:19.
-