-
Kujitahidi Kuwa WashindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
3. (a) Ni kitia-moyo gani ambacho Yesu aliwapa Wakristo katika Smirna? (b) Ingawa Wakristo katika Smirna walikuwa maskini, ni kwa nini Yesu alisema wao walikuwa ‘matajiri’?
3 “Mimi najua dhiki na umaskini wako—lakini wewe u tajiri—na kufuru la wale ambao husema wao wenyewe ni Wayahudi, na kumbe wao sio bali ni sinagogi la Shetani.” (Ufunuo 2:9, NW) Yesu hana uchambuzi kwa ndugu zake katika Smirna, ana pongezi changamfu tu. Wao wamepatwa na dhiki nyingi sana kwa sababu ya imani yao. Kimwili wao ni maskini, yaelekea kwa sababu ya uaminifu wao. (Waebrania 10:34) Hangaikio lao kuu, hata hivyo, ni vitu vya kiroho, nao wamejiwekea akiba hazina katika mbingu, kama Yesu alivyoshauri. (Mathayo 6:19, 20) Kwa sababu hiyo, Mchungaji Mkuu anawaona wao kuwa “tajiri.”—Linga Yakobo 2:5.
4. Wakristo katika Smirna walipatwa na upinzani mwingi sana kutoka kwa nani, naye Yesu aliwaonaje wapinzani hao?
4 Yesu anataja hasa kwamba Wakristo katika Smirna wamechukuana na upinzani mwingi mikononi mwa Wayahudi wa kimnofu. Katika siku za mapema zaidi, wengi wa dini hii walipinga kwa dhati kuenea kwa Ukristo. (Matendo 13:44, 45, 14:19) Sasa, miongo michache tu baada ya Yerusalemu kuanguka, Wayahudi hao katika Smirna wanaonyesha roho ile ile ya kishetani. Si ajabu kwamba Yesu anawaona hao kuwa “sinagogi la Shetani”!a
-
-
Kujitahidi Kuwa WashindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
a Yapata miaka 60 baada ya Yohana kufa, Polycarp mwenye umri wa miaka 86 aliteketezwa mpaka kifo katika Smirna kwa sababu yeye hangeweza kukana itikadi yake katika Yesu. The Martyrdom of Polycarp, kitabu kinachoitikadiwa kuwa cha wakati ule ule mmoja na tukio hili, hutaarifu kwamba wakati kuni zilipokuwa zikikusanywa za kuteketeza yeye, “wale Wayahudi walikuwa na bidii kupita kiasi, kama ilivyo desturi yao, katika kusaidia katika hili”—hata ingawa kufishwa huko kulitukia katika “siku kubwa ya Sabato.”
-