-
Mwanavita-Mfalme Asherehekea Ushindi Kwenye Har–MagedoniUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Macho yake ni mwali wa moto, na juu ya kichwa chake pana mataji mengi.”—Ufunuo 19:11, 12a, NW.
-
-
Mwanavita-Mfalme Asherehekea Ushindi Kwenye Har–MagedoniUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Macho yake yanavuvia hofu, kama “mwali wa moto,” akitarajia uharibifu wenye moto unaokuja wa maadui wake.
6 Mataji mengi hupamba kichwa cha Mwanavita-Mfalme huyu. Hayawani-mwitu ambaye Yohana aliona akitoka katika bahari alikuwa na mataji kumi, yakiwa ni picha ya utawala wake wa kitambo wa mandhari ya kidunia. (Ufunuo 13:1, NW) Ingawa hivyo, Yesu ana “mataji mengi.” Utawala wake wenye utukufu haulandiki, kwa kuwa yeye ni “Mfalme wa wale ambao hutawala wakiwa wafalme na Bwana wa wale ambao hutawala wakiwa mabwana.”—1 Timotheo 6:15, NW.
7. Jina lililoandikwa alilo nalo Yesu ni jipi?
7 Elezo la Yohana laendelea: “Yeye ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mmoja ajuaye ila yeye mwenyewe.” (Ufunuo 19:12b, NW) Tayari Biblia husema juu ya Mwana wa Mungu kwa majina kama Yesu, Imanueli, na Mikaeli. Lakini “jina” lake lisilotajwa laonekana kuwa lasimamia cheo na mapendeleo ambayo Yesu anafurahia wakati wa siku ya Bwana. (Linga Ufunuo 2:17.) Isaya, akieleza habari ya Yesu tangu 1914, anasema: “Jina lake ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mwana-Mfalme wa Amani.” (Isaya 9:6, NW) Mtume Paulo alishirikisha jina la Yesu na mapendeleo ya juu sana ya utumishi wakati alipoandika: “Mungu alimkweza [Yesu] kwenye cheo cha juu sana na kwa fadhili akampa yeye jina ambalo liko juu ya kila jina jingine, ili kwamba katika jina la Yesu kila goti lipaswe kupigwa.”—Wafilipi 2:9, 10, NW.
8. Ni kwa sababu gani ni Yesu tu anayeweza kujua hilo jina lililoandikwa, na yeye anashiriki na nani baadhi ya mapendeleo yake ya juu sana?
8 Mapendeleo ya Yesu hayana kifani. Isipokuwa Yehova mwenyewe, ni Yesu tu anayeweza kufahamu linalomaanishwa na kuwa na cheo kama hicho cha juu. (Linga Mathayo 11:27.) Kwa hiyo, kati ya viumbe wote wa Mungu, ni Yesu tu anayeweza kuthamini jina hilo. Hata hivyo, Yesu anatia ndani bibi-arusi wake katika baadhi ya mapendeleo haya. Kwa hiyo yeye anatoa ahadi hii: “Yeye ambaye hushinda . . . mimi nitaandika juu ya yeye . . . hilo jina jipya langu.”—Ufunuo 3:12, NW.
-