-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Na yeye akakamata drakoni, nyoka wa awali kabisa, ambaye ndiye Ibilisi na Shetani, na akamboba yeye kwa miaka elfu moja.
-
-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
5. Malaika wa abiso hushughulikaje na Shetani Ibilisi, na kwa nini?
5 Drakoni mkubwa mwenye rangi-moto alipovurumishwa chini kutoka katika mbingu, alisemwa kuwa ndiye “nyoka wa awali kabisa, mmoja ambaye huitwa Ibilisi na Shetani, ambaye anaongoza vibaya dunia nzima yote inayokaliwa.” (Ufunuo 12:3, 9, NW) Sasa, wakati wa kukamatwa kwake na kutiwa ndani ya abiso, yeye ameelezwa tena kwa ukamili kuwa ndiye “drakoni, nyoka wa awali kabisa, ambaye ndiye Ibilisi na Shetani.” Huyu ambaye ni mmezaji, mdanganyaji, mchongezi, na mpinzani mwenye sifa mbaya sana anafungwa mnyororo na kuvurumishwa “ndani ya abiso,” ambayo inashindikwa ndi ndi ndi na kutiwa kalafati kikiki, “ili asipate kuongoza vibaya mataifa tena.” Huku kutiwa kwa Shetani ndani ya abiso ni kwa muda wa miaka elfu moja, wakati huo uvutano wake juu ya aina ya binadamu utakuwa haupo tena kama wa mfungwa aliye ndani ya gereza la shimo lenye kina kirefu. Malaika wa abiso anamwondolea mbali kabisa Shetani asiwe na mgusano wowote na Ufalme wa uadilifu. Lo! ni kitulizo kama nini kwa aina ya binadamu!
-