Maeneo Walikoishi Wazee Wa Ukoo
STEFANO alianza hotuba yake inayojulikana kwa kutaja maeneo fulani hususa: “[Yehova] alimtokea babu yetu Abrahamu alipokuwa Mesopotamia, kabla ya kuanza kukaa Harani, naye akamwambia, ‘Toka . . . uje mpaka katika nchi ambayo nitakuonyesha.’” (Mdo 7:1-4) Kutii amri hiyo kuliongoza kwenye matukio muhimu katika Nchi ya Ahadi yaliyohusu Abrahamu, Isaka, na Yakobo, na yaliyohusiana na kusudi la Mungu la kuwabariki wanadamu.—Mwa 12:1-3; Yos 24:3.
Mungu alimwita Abrahamu (au Abramu) kutoka Uru la Wakaldayo, jiji lenye ufanisi ambalo wakati huo lilikuwa upande wa mashariki wa ukingo wa Mto Efrati. Abrahamu angepitia njia gani? Kutoka eneo la Ukaldayo, ambalo pia liliitwa Shinari, ingekuwa rahisi kuelekea moja kwa moja magharibi. Kwa nini aelekee kaskazini hadi Harani?
Jiji la Uru lilikuwa karibu na mashariki mwa Eneo Lenye Rutuba ambalo lilianzia Palestina hadi maeneo yaliyo katikati ya mito ya Tigri na Efrati. Huenda hapo awali eneo hilo halikuwa kame sana wala halikuwa na joto jingi. Upande wa kusini wa eneo hilo, kulikuwa na Jangwa la Siria lenye vilima vya mawe ya chokaa na nchi tambarare za mchanga. Kichapo The Encyclopædia Britannica kinasema kwamba eneo lililokuwa kati ya Pwani ya Mediterania na Mesopotamia “halingeweza kupitika kwa urahisi.” Huenda misafara fulani ya wafanyabiashara walikuwa wakivuka jangwa hilo kutoka Mto Efrati kwenda Tadmori, kisha Damasko. Lakini Abrahamu na familia yake pamoja na mifugo yao hawakupitia njia hiyo ya jangwani.
Badala yake, Abrahamu alipitia bonde la Mto Efrati akielekea Harani. Kutoka hapo, alipitia njia iliyotumiwa na wafanyabiashara, akavuka mto huko Karkemishi, kisha akaelekea upande wa kusini karibu na Damasko hadi kwenye eneo ambalo sasa ni Bahari ya Galilaya. “Njia ya Baharini” au Via Maris, ilipitia Megido hadi Misri. Hata hivyo, Abrahamu alisafiri kupitia milima ya Samaria na hatimaye akapiga hema huko Shekemu. Baada ya muda, alielekea kusini akipitia eneo hilo lenye milima. Unaweza kufuata njia aliyopitia kwenye ramani unaposoma Mwanzo 12:8-13:4. Ona maeneo mbalimbali aliyopitia: Dani, Damasko, Hoba, Mamre, Sodoma, Gerari, Beer-sheba, na Moria (Yerusalemu).—Mwa 14:14-16; 18:1-16; 20:1-18; 21:25-34; 22:1-19.
Kufahamu baadhi ya maeneo hayo kutakusaidia kuelewa vizuri zaidi matukio fulani katika maisha ya Isaka na Yakobo. Kwa mfano, Abrahamu alipokuwa Beer-sheba, alimtuma mtumishi wake wapi amtafutie Isaka mke? Alielekea kaskazini kupitia Mesopotamia (jina linalomaanisha, “Eneo Lililo Katikati ya Mito Miwili”) hadi Padan-aramu. Kisha wazia safari yenye kuchosha aliyofunga Rebeka akitumia ngamia kwenda kukutana na Isaka huko Negebu, labda karibu na Kadeshi.—Mwa 24:10, 62-64.
Baadaye Yakobo (Israeli) mwana wa Isaka na Rebeka alifunga safari ndefu kama hiyo kwenda kumwoa mwabudu wa Yehova. Lakini Yakobo alipitia njia tofauti kidogo alipokuwa akirudi nchini kwao. Baada ya kuvuka Mto Yaboki karibu na Penueli, Yakobo alipigana mweleka na malaika. (Mwa 31:21-25; 32:2, 22-30) Esau alikutana na Yakobo huko, kisha kila mmoja wao akaenda kuishi eneo tofauti.—Mwa 33:1, 15-20.
Baada ya Dina binti ya Yakobo kulalwa kinguvu huko Shekemu, Yakobo alihamia Betheli. Je, unajua wana wa Yakobo walisafiri umbali gani kwenda kulisha mifugo ya baba yao, naye Yosefu aliwapata wapi hatimaye? Ramani hii (na ile iliyo kwenye ukurasa wa 18 na 19) inaweza kukusaidia kujua Betheli ilikuwa umbali gani na Dothani. (Mwa 35:1-8; 37:12-17) Ndugu za Yosefu walimwuza kwa wafanyabiashara waliokuwa wakielekea Misri. Unafikiri wafanyabiashara hao walipitia njia gani walipompeleka Yosefu Misri akiwa mtumwa, jambo ambalo liliweka msingi wa Waisraeli kuhamia Misri na baadaye kutoka huko?—Mwa 37:25-28.
[Ramani katika ukurasa wa 7]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Safari za Abrahamu (see publication)
Safari za Isaka (see publication)
Safari za Yakobo (see publication)
Barabara Kuu (see publication)
Wazee wa Ukoo
A4 GOSHENI
A5 MISRI
B4 SHURI
B5 PARANI
C3 Damasko
C3 Dani (Laishi)
C4 Shekemu
C4 Betheli
C4 Hebroni (Kiriath-arba)
C4 Gerari
C4 Beer-sheba
C4 SEIRI
C4 Kadeshi
C5 EDOMU
D1 Karkemishi
D2 Tadmori
D3 Hoba
E1 PADAN-ARAMU
E1 Harani
F2 MESOPOTAMIA
G1 Ninawi
G2 ENEO LENYE RUTUBA
G3 Babiloni
H4 UKALDAYO
H4 Uru
[Milima]
C4 Moria
[Bahari]
B3 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)
[Mito]
Efrati
Tigri
[Wazee wa Ukoo (katika Nchi ya Ahadi)
KANAANI
Megido
GILEADI
Dothani
Shekemu
Sukothi
Mahanaimu
Penueli
Betheli (Luzi)
Ai
Yerusalemu (Salemu)
Bethlehemu (Efrathi)
Mamre
Hebroni (Makpela)
Gerari
Beer-sheba
Sodoma?
NEGEBU
Rehobothi?
Beer-lahai-roi
Kadeshi
[Babara Kuu]
Via Maris
Barabara ya Mfalme
[Milima]
Moria
[Bahari]
Bahari ya Chumvi
[Mito na Kijito]
Yaboki
Yordani
[Picha katika ukurasa wa 6]
Mto Efrati karibu na Babiloni
[Picha katika ukurasa wa 6]
Abrahamu aliishi Beer-sheba na alilisha mifugo yake katika maeneo yaliyokuwa karibu
[Picha katika ukurasa wa 6]
Bonde la mto la Yaboki