-
Rekodi ya Kale ya Uumbaji—Je, Unaweza Kuitumaini?Je, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
“Siku” ya Pili na ya Tatu
Kabla ya Muumba kufanya nchi kavu itokee katika “siku” ya tatu ya uumbaji, yeye aliinua baadhi ya maji. Tokeo likawa kwamba dunia ilifunikwa kwa mvuke wa maji.c Hiyo rekodi ya kale haisemi—wala haihitaji kusema—njia iliyotumiwa. Badala yake, Biblia yakazia nafasi iliyopo baina ya maji ya juu na maji yaliyo kwenye uso wa dunia. Inaita nafasi hiyo mbingu. Hata leo watu hutumia neno hilo kumaanisha anga ambamo ndege hupaa. Baada ya muda, Mungu alijaza mbingu hiyo kwa gesi tofauti-tofauti zilizo muhimu kwa uhai.
-
-
Rekodi ya Kale ya Uumbaji—Je, Unaweza Kuitumaini?Je, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
c Huenda Muumba alitumia njia za asili ili kuinua maji hayo na kuyadumisha huko juu. Maji hayo yalinyesha katika siku za Noa. (Mwanzo 1:6-8; 2 Petro 2:5; 3:5, 6) Tukio hili la kihistoria liliathiri sana wanadamu waliookoka na wazao wao, kama vile wataalamu wa kuchunguza asili ya wanadamu wawezavyo kuthibitisha. Tukio hilo limeonyeshwa katika masimulizi yaliyohifadhiwa na watu duniani pote.
-