-
Je, Maandishi ya Noa Yana Maana Kwetu?Mnara wa Mlinzi—2003 | Mei 15
-
-
Sasa huenda ukataka kusoma Mwanzo 8:5-17. Vilele vya milima vilianza kuonekana karibu miezi miwili na nusu (siku 73) baadaye, ‘mwezi wa kumi [Juni], siku ya kwanza ya mwezi.’ (Mwanzo 8:5)b Miezi mitatu [siku 90] baadaye—katika “mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza” ya maisha ya Noa, au katikati ya mwezi wa Septemba, 2369 K.W.K., Noa aliondoa kifuniko cha safina. Hivyo angeweza kuona kwamba “uso wa nchi umekauka.” (Mwanzo 8:13) Mwezi mmoja na siku 27 (siku 57) baadaye, “mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi [katikati ya mwezi wa Novemba, 2369 K.W.K.], nchi ilikuwa kavu.” Kwa hiyo Noa na familia yake wakatoka nje kwenye nchi kavu. Hivyo, Noa na wengine walikaa ndani ya safina kwa mwaka mmoja na siku kumi (siku 370).—Mwanzo 8:14.
-
-
Je, Maandishi ya Noa Yana Maana Kwetu?Mnara wa Mlinzi—2003 | Mei 15
-
-
b Kichapo Commentary on the Old Testament cha Keil-Delitzsch, Buku la 1, ukurasa wa 148 kinasema: “Yaelekea baada ya siku 73 vilele vya milima ya Armenia iliyoizunguka safina vilionekana.”
-