-
Toleo la Hiari ili Kuendeleza Ibada SafiMnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 1
-
-
Waisraeli walikuwa na vitu vya kutosha kuweza kutoa mchango kama huo wa ukarimu. Kumbuka kwamba walipotoka Misri walichukua vito vya dhahabu na fedha pamoja na nguo nyingi. Kwa kweli, “wakawateka Wamisri nyara.”a (Kutoka 12:35, 36) Hapo awali, Waisraeli walikuwa wametoa vito vyao kwa hiari ili kutengeneza sanamu kwa ajili ya ibada isiyo ya kweli. Je, sasa wangeonyesha hamu hiyohiyo katika kutoa michango ya kuendeleza ibada ya kweli?
-
-
Toleo la Hiari ili Kuendeleza Ibada SafiMnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 1
-
-
a Huo haukuwa wizi. Waisraeli waliomba michango kutoka kwa Wamisri, wakapewa kwa hiari. Isitoshe, kwa kuwa Wamisri hawakuwa na haki ya kuwafanya Waisraeli watumwa, walipaswa kuwalipa watu wa Mungu mishahara kwa kazi ngumu waliyokuwa wamefanya kwa miaka mingi.
-