-
Amri Kumi Zina Maana Gani Kwako Wewe?Mnara wa Mlinzi—1989 | Novemba 15
-
-
Kufuata hapo, Yehova alimpa Musa maagizo katika amri nyingine za kimungu kwa Israeli. (Kutoka 20:4–23:19) Zote pamoja, zilijumlika kuwa sheria kama 600. Nao ulikuwa msisimuko ulioje kung’amua kwamba malaika wa Mungu alikuwa akienda mbele ya taifa ili kutayarisha njia ya kuingia katika Bara la Ahadi! (Kutoka 23:20-22) Yehova alijulisha wazi hivi: “Mimi nitafanya mbele ya watu wako wote mambo ya ajabu ambayo hayajafanyizwa kamwe katika dunia yote wala miongoni mwa mataifa yote; na watu wote ambao wewe upo katikati yako wataiona kazi ya Yehova, kwa sababu ni jambo lenye kuvuvia hofu ambalo mimi ninafanya kwa habari ya nyinyi.” Mungu alitaka watu wake nao wamrudishie nini? “Wewe nawe kwa sehemu yako shika jambo ambalo mimi ninakuamuru leo.” Ndiyo, utii kwa sheria na miongozo yote ya Yehova uliamrishwa.—Kutoka 34:10, 11, NW.
-
-
Amri Kumi Zina Maana Gani Kwako Wewe?Mnara wa Mlinzi—1989 | Novemba 15
-
-
Lakini namna gani kuhusu ile amri ya nne, ambayo yahusiana na siku ya Sabato? Amri hii ilikazia kustahi mambo matakatifu, kama vile Yehova alivyokuwa ameonyesha alipokuwa akianzisha “mwadhimisho wa sabato” kuhusiana na kukusanya mana. (Kutoka 16:22-26) Kwa sababu Waisraeli fulani hawakutii haraka, Yehova aliwakumbusha wazi kwamba yeye ndiye alikuwa amewapa agizo hilo. “‘Ukumbukeni vizuri uhakika wa kwamba Yehova ndiye amewapa nyinyi ile sabato.’ . . . Na watu wale wakafuliza kushika sabato siku ya saba.” (Kutoka 16:29, 30, NW) Baadaye, Yehova alionyesha jinsi mpango huu usivyohusisha wengine ndani, akitaarifu hivi: “Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli kwa wakati usio dhahiri.”—Kutoka 31:17, NW.
-
-
Amri Kumi Zina Maana Gani Kwako Wewe?Mnara wa Mlinzi—1989 | Novemba 15
-
-
Amri nne za kwanza zakazia madaraka yetu kuelekea Yehova. (Ya Kwanza) Yeye ni Mungu ambaye bado atoza ujitoaji wa pekee. (Mathayo 4:10, NW) (Ya Pili) Hakuna yeyote wa waabudu wake apaswa kutumia mifano ya ibada. (1 Yohana 5:21) (Ya Tatu) Utumizi wetu wa jina la Mungu wapaswa kuwa ufaao na wenye heshima nyingi, si wenye utovu wa staha kamwe. (Yohana 17:26; Warumi 10:13) (Ya Nne) Maisha yetu yote yapasa yawe na tegemeo lenye kuzungukia mambo matakatifu. Hii yatuwezesha sisi kupumzika, au ‘tuchukue sabato,’ kutoka kwenye mwendo wa kujihesabia uadilifu.—Waebrania 4:9, 10, NW.
-