MWAKA
Sha·nahʹ ni neno la msingi la Kiebrania kwa ajili ya “mwaka” nalo linatokana na mzizi wa maneno unaomaanisha “rudia; fanya tena” na, kama tu neno la Kigiriki linalofanana na hilo e·ni·au·tosʹ, linabeba wazo la mzunguko wa wakati. Kutokea tena kwa misimu mipya ndiko kunakoashiria kwa wazi kukamilika kwa vipindi vya mwaka duniani; na kwa upande mwingine misimu inaongozwa na mizunguko ya dunia inapolizunguka jua. Kwa hiyo, Muumba ameandaa njia ya kupima wakati kupitia miaka kwa kuiweka dunia katika mzunguko wake, huku mhimili wa dunia ukiwekwa katika pembe inayofaa kuhusiana na usawa wa mwendo wake wa kulizunguka jua. Pia, njia inayotegemeka ya kugawanya mwaka katika vipindi vidogo-vidogo imeandaliwa kupitia utaratibu wa mzunguko wa mwezi. Kanuni hizi zilionyesha mapema katika masimulizi ya Biblia.— Mwa 1:14-16; 8:22.
Tangu mwanzoni, mwanadamu ametumia viashiria hivyo vilivyoandaliwa na Mungu kupima wakati kwa kutegemea miaka iliyogawanywa kwa miezi. (Mwa 5:1-32) Watu wengi wa kale walitumia mwaka wenye miezi 12. Mwaka wa kawaida unaotegemea kuonekana kwa mwezi una siku 354, zikiwa na miezi yenye siku 29 au 30, ikitegemea kujitokeza kwa kila mwezi mpya. Kwa hiyo, kuna siku 11 1⁄4 hivi zinazopungua kwa kulinganisha na mwaka sahihi unaotegemea jua //mwaka wa jua wenye siku 365 1⁄4 (siku 365 saa 5 dakika 48 na sekunde 46)).
Katika Siku za Noa. Katika siku za Noa tunapata rekodi ya kwanza ya kale ya kuhesabu urefu wa mwaka. Ni wazi kwamba aligawanya mwaka katika miezi 12 yenye siku 30 kila mmoja. Kwenye Mwanzo 7:11, 24 na 8:3-5 “orodha” ambayo Noa alitunza inaonyesha siku 150 kuwa ni sawa na miezi mitano. Katika simulizi hilo, mwezi wa pili, wa saba na wa kumi wa mwaka wa Gharika inatajwa moja kwa moja. Kisha, baada ya mwezi wa kumi na siku yake ya kwanza, kipindi cha siku 40 kinatokea, pamoja na vipindi viwili vya siku 7 kila kimoja, au jumla ya siku 54. (Mwa 8:5-12) Pia, kuna kipindi chenye urefu usiojulikana kati ya wakati kunguru alipotumwa hadi wakati njiwa alipotumwa kwa mara ya kwanza. (Mwa 8:6-8) Vilevile, kipindi kingine chenye urefu usiojulikana kinaonyeshwa kwenye Mwanzo 8:12 njiwa alipotumwa kwa mara ya tatu na ya mwisho. Katika mstari unaofuata, tunaona siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wa mwaka unaofuata ikitajwa. (Mwa 8:13) Haijulikani ni njia gani iliyotumiwa na Noa au wale walioishi kabla yake kusawazisha mwaka uliofanyizwa kwa miezi yenye siku 30 na mwaka unaotegemea jua.
Misri na Babiloni. Katika Misri ya kale, mwaka ulifanyizwa kwa miezi 12 yenye siku 30 kwa kila mmoja, na siku tano za ziada ziliongezwa kila mwaka ili kufanya mwaka uende sambamba na mwaka unaotegemea jua. Kwa upande mwingine, Wababiloni walishikamana na mwaka unaotegemea mwezi, lakini waliongeza mwezi wa 13, unaoitwa Veadar, katika baadhi ya miaka, ili misimu iende sambamba na miezi ambayo kwa kawaida ingeendana. Mwaka kama huo unaitwa mwaka unaotegemea mwezi na jua // mwaka wa mwezi wa ki-anga na jua na kihalisi pindi fulani mwaka huo huwa mfupi au mrefu kuliko mwaka halisi unaotegemea jua, hususan ikiwa mwaka unaotegemea mwezi una miezi 12 au 13.
Mzunguko wa Miaka 19. Baada ya muda fulani mfumo wa kuweka mwezi wa nyongeza, au wa 13, mara saba kila baada ya miaka 19 ulianzishwa, na kutoa matokeo yanayokaribiana sana na miaka 19 iliyo halisi inayotegemea jua. Mzunguko huo ulikuja kupewa jina la Meton mwanahisabati wa karne ya tano K.W.K.
Waebrania. Biblia haisemi ikiwa njia hii ndiyo hasa iliyotumiwa na Waebrania kusawazisha mwaka wao uliotegemea mwezi na ule unaotegemea jua. Uthibitisho wa kwamba majina yaliyonakiliwa ya miezi yao ni majina ya misimu unaonyesha kwamba walitumia njia fulani ya kusawazisha. Mara mbili kila mwaka jua huvuka mstari wa ikweta, na katika pindi hizo ulimwenguni pote usiku na mchana huwa na urefu sawa (saa 12 hivi za mwangaza na saa 12 hivi za giza). Pindi hizo mbili huitwa mwanzo wa masika au siku mlingano na majira ya kupukutika au siku mlingano. Hilo hutokea tarehe 21 hivi Machi na 23 hivi Septemba katika kila mwaka wa kalenda yetu. Kutokea huko kwa siku mlingano kungetokeza njia ya kujua wakati ambapo mwezi halisi unaotumiwa kuhesabu miezi ungekuwa mbele sana na misimu iliyohusiana nayo na hivyo ingetumiwa kama mwongozo wa kufanya marekebisho yaliyohitajiwa kwa kuweka mwezi wa nyongeza.
Zamani, miaka ilihesabiwa ikijiudia kwanzia majira ya kupukutika hadi majira mengine ya kupukutika, mwezi wa kwanza ukianzia karibu na katikati ya mwezi wetu wa Septemba wa sasa. Hilo linalingana na mapokeo ya Kiyahudi kwamba mwanadamu aliumbwa katika majira ya kupukutika. Kwa kuwa Biblia ina rekodi ya umri wa Adamu kwa njia ya miaka (Mwa 5:3-5), inapatana na akili kwamba hesabu zilianza kufanywa kuanzia wakati wa kuumbwa kwake, na ikiwa kwa kweli aliumbwa katika majira ya kupukutika, hilo litatoa ufafanuzi kwa kiasi fulani zoea la kale la kuanza mwaka mpya katika majira hayo. Kwa kuongezea, hata hivyo, mwaka kama huo ungefaa kabisa maisha ya ukulima ya watu, hasa kwenye sehemu ya dunia ambapo watu wa kabla ya Gharika na mapema baada ya Gharika waliishi. Mwaka uliisha katika kipindi cha mavuno ya mwisho na kuanza na kulima na kupanda mbegu kuelekea sehemu ya mwanzoni ya mwezi wetu wa Oktoba.
Mwaka mtakatifu na wa kawaida// wa kilimwengu. Mungu alibadili mwanzo wa miaka kwa taifa la Israeli kipindi Walipotoka Misri, akawaagiza kwamba mwaka ungepaswa kuanza katika mwezi wa Abibu, au Nisani, wakati wa masika. (Kut 12:1-14; 23:15) Hata hivyo, bado majira ya kupukutika yalitumiwa kuashiria mwanzo wa mwaka wao wa kawaida au kilimo. Hivyo, kwenye Kutoka 23:16, Sherehe ya Kukusanya, ambayo ilifanywa wakati wa masika katika mwezi wa Ethanimu, mwezi wa saba wa kalenda takatifu, inatajwa kuwa ilifanyika “mwishoni mwa mwaka” na kwenye Kutoka 34:22 kama “mwishoni mwa mwaka.” Pia, mwongozo uliohusiana na miaka ya kuadhimisha Mwadhimisho wa Miaka 50 unaonyesha kwamba ilihesabiwa kuanzia majira ya kupukutika ya mwezi wa Ethanimu.—Law 25:8-18.
Yosefo, mwanahistoria Myahudi (wa karne ya kwanza W.K.) alisema kwamba mwaka mtakatifu (ulioanza katika majira ya kupukutika) ulitumiwa kuhusiana na sherehe za kidini lakini mwaka halisi wa kawaida (ulioanza wakati wa masika) uliendelea kutumiwa kuhusiana na kununua, kuuza, na masuala mengine ya kawaida. (Jewish Antiquities, I, 81 [iii, 3]) Mifumo hii miwili ya mwaka mtakatifu na mwaka wa kawaida ni maarufu katika kipindi cha baada ya kutoka uhamishoni kufuatia Wayahudi kuachiliwa kutoka Babiloni. Siku ya kwanza ya Nisani, au Abibu, iliashiria mwanzo wa mwaka mtakatifu, na siku ya kwanza ya Tishri, au Ethanimu, iliashiria mwanzo wa mwaka wa kawaida. Katika kila kisa, ule ambao ulikuwa mwezi wa kwanza wa kalenda hii ulikuja kuwa wa saba kwenye ile kalenda nyingine.— Ona KALENDA.
Kalenda inayopatana//inayowiana na sherehe. Matukio muhimu zaidi ya kila mwaka yalikuwa vipindi vitatu vikubwa sana ya sherehe vilivyoamriwa na Yehova Mungu: Pasaka (iliyofuatiwa na Sherehe ya Mikate Isiyo na Chachu) kwenye Nisani 14; Sherehe ya Majuma, au Pentekoste, kwenye Sivani 6; na Sherehe ya Kukusanya (ilitanguliwa na Siku ya Kufunika Dhambi) kwenye Ethanimu 15-21. Sherehe ya Mikate Isiyo na Chachu ilishabihiana na mavuno ya shayiri, Pentekoste na mavuno ya ngano, na Sherehe ya Kukusanya na mavuno ya ujumla mwishoni mwa mwaka wa kilimo.
Miaka ya Sabato na Mwadhimisho wa Miaka 50. Chini ya agano la Sheria, kila mwaka wa saba ulikuwa mwaka wa pumziko kamili kwa ardhi, mwaka wa Sabato. Kipindi au wiki ya miaka ya saba viliitwa ‘miaka ya sabato.’ (Law 25:2-8) Kila mwaka wa 50 ulikuwa mwaka wa Mwadhimisho wa Miaka 50 wa kupumzika, ambao watumwa wote Waebrania waliachiliwa huru na ardhi yoyote iliyotokana na urithi ilirudishwa kwa wamiliki wake halisi.—Law 25:10-41; see MWAKA WA SABATO.
Njia ya kuhesabu utawala wa wafalme. Katika rekodi za kihistoria, lilikuwa zoea la kawaida nchini Babiloni kuhesabu miaka ya utawala wa mfalme kama miaka kamili, kuanzia Nisani 1. Miezi ambayo kihalisi mfalme alianza kutawala kabla ya Nisani 1 ilionwa kuwa iliunda mwaka wa kupokea mamlaka, lakini kihistoria miaka hiyo ilipewa, au kuhesabiwa kama miaka kamili ya mfalme aliyetangulia. Ikiwa, kama mapokeo ya Kiyahudi yanavyoonyesha, mfumo huo ulifuatwa huko Yuda, basi, Biblia inapozungumzia kuhusu Mfalme Daudi na Sulemani kwamba kila mmoja alitawala kwa “miaka 40,” utawala wao ulihusisha vipindi miaka 40 kamili.—1Fa 1:39; 2:1, 10, 11; 11:42.
Katika Unabii. Katika unabii kwa kawaida neno “mwaka” linatumiwa katika njia ya pekee likiwa sawa na siku 360 (miezi 12 yenye siku 30 kila mmoja). (Ufu 11:2, 3) Pia, unaitwa “wakati” na pindi fulani unawakilishwa kwa njia ya mfano na “siku.”—Ufu 12:6, 14; Eze 4:5, 6.