-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—2000 | Oktoba 15
-
-
Yehova, ambaye ndiye chanzo cha uhai wetu, alikataza ulaji wa damu. (Mwanzo 9:3, 4) Katika Sheria aliyowapa Waisraeli wa kale, Mungu alikataza matumizi ya damu kwa kuwa inawakilisha uhai. Aliamuru hivi: “Uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.” Namna gani ikiwa mtu aliua mnyama kwa ajili ya chakula? Mungu alisema: “Atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga.”a (Mambo ya Walawi 17:11, 13) Yehova alirudia amri hiyo tena na tena. (Kumbukumbu la Torati 12:16, 24; 15:23) Kichapo cha Kiyahudi, Soncino Chumash, chasema: “Damu haipasi kuwekwa akiba lakini yapasa kumwagwa chini ili isifae kuliwa.” Hakuna Mwisraeli aliyepaswa kutwaa, kuweka akiba, na kutumia damu ya kiumbe mwingine, ambaye uhai wake ulitoka kwa Mungu.
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—2000 | Oktoba 15
-
-
Mara kwa mara, daktari atamhimiza mgonjwa kuweka akiba ya damu yake mwenyewe majuma kadhaa kabla ya upasuaji ili ikihitajika, aweze kumtia mgonjwa huyo damu yake mwenyewe iliyowekwa akiba. Lakini kutoa damu hiyo, kuiweka akiba, na kuitia mishipani hupingana moja kwa moja na yale yasemwayo katika kitabu cha Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Damu haipasi kuwekwa akiba; yapasa kumwagwa—kana kwamba kuirudisha kwa Mungu. Ni kweli kwamba Sheria ya Kimusa haitumiki sasa. Hata hivyo, Mashahidi wa Yehova wanaheshimu kanuni za Mungu zilizo katika sheria hiyo, nao wameazimia ‘kujiepusha na damu.’ Kwa hiyo, hatutoi damu, wala hatuweki akiba damu yetu kwa ajili ya kutiwa mishipani kwa sababu yapasa ‘kumwagwa.’ Kutoa damu au kuiweka akiba hupingana na sheria ya Mungu.
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—2000 | Oktoba 15
-
-
a Profesa Frank H. Gorman aandika: “Kumwaga damu kunaeleweka vizuri kuwa kitendo cha staha kinachodhihirisha heshima kwa uhai wa mnyama, na hivyo heshima kwa Mungu, aliyeumba na anayeendelea kuutunza uhai huo.”
-