Mandhari Kutoka Bara la Ahadi
Kutoka Tabori Kusonga Mbele Hadi Ushindi
WAZIA ukiwa katika mnara ukitazama chini mahali ambapo vijia vya historia vilipitana! Kwa kweli ungeweza kuwa ni kama unashuhudia kutendeka kwa yaliyofanyika katika historia.
Mahali pa Kibiblia ambapo Megido ilikuwa pangeweza kufaana kabisa na maelezo hayo, kwa maana palitagaa (upande huu na huu) kwenye njia muhimu za kibiashara na kijeshi. Hata hivyo, ng’ambo ya Bonde la Yezreeli upo Mlima Tabori, ambao pia ulitazama chini juu ya Via Maris, ile njia yenye sifa ya kwenda kwenye majiji ya Hilali (Eneo) Yenye Rutuba.a
Ukitazama Tabori ukiwa karibu mahali popote katika jimbo hilo, hata iweje utavutiwa tu. (Linganisha Yeremia 46:18.) Tabori huinuka kwa uvutio wenye kutofautiana sana na mazingira yao, huku umbo lao lenye kuchongoka kama pia likitambulika kutoka pande zote. Mlima huo huinuka juu ya uwanda wenye kusambaa mbele yao upande wa kusini, lile Bonde la Yezreeli lenye rutuba, ambalo huunganisha pwani na Bonde la Yordani.
Ukiwa kwenye kilele kilichoviringika kwa uanana cha Tabori, waweza kutazama kusini kuelekea jiji la Yezreeli, na hiyo huenda ikakukumbusha juu ya mpando wenye kiruu kingi wa Yehu akielekea kwenye kao la kifalme la Ahabu na juu ya mwisho wenye fedheha wa Yezebeli. (1 Wafalme 21:1; 2 Wafalme 9:16-33) Hapo karibu ni Megido. Kuelekea magharibi waweza kuona Mlima Karmeli, ambapo Eliya alifanya ule mtihani wa moto. (1 Wafalme, sura ya 18) Ukiwa Tabori waweza pia kuona mahali ambapo mto Kishoni hutiririka kuelekea bahari, na zapata kilometa 8 magharibi ya kaskazini-magharibi katika vilima vya Galilaya ya chini ni Nazareti.
Lakini kutajwa kwa Tabori kwakukumbusha usimulizi gani wa Biblia? Yaelekea ni ule wa Debora na Baraka. Katika wakati wao, Wakanaani wakiwa chini ya Mfalme Yabini wa Hazori walikuwa wameonea Israeli kwa miaka 20. Ndipo Debora nabii wa kike akachochea Baraka kuchukua hatua. Baraka, naye, akawapa moyo Waisraeli kumi elfu, sana-sana wa kabila la Naftali na Zebuluni katika Galilaya, na kuwakusanya juu ya Tabori. Silaha zao hazikuwa nzuri sana, kwa maana hakukuwa na hata ngao moja wala fumo moja katika Israeli.—Waamuzi 5:7-17.
Songamano kubwa sana la kijeshi likaja dhidi yao. Sisera jemadari wa Yabini alileta mashujaa-vita Wakanaani wenye silaha nyingi kwenye Bonde la Yezreeli. Ni lazima wawe walionekana kidogo kama wanaume wenye silaha walioonyeshwa katika ule mchongeleo wa ukutani uliotoka Misri ambao umefanyiwa kielezi katika ukurasa ufuatao, juu kulia. Vyombo vya vita vya Misri vilihusika kuamua vile vyenye kutumiwa katika Kanaani, kutia na sehemu iliyo ya kuogopesha sana ya silaha za Sisera—magari-vita 900!
Magari-vita hayo ya Kikanaani yangalikuwa ni majukwaa yenye kwenda huku na huku ya kutupia silaha. Dreva angeweza kuwa alizifungia hatamu kuzunguka kiuno chake ili mikono yake iwe huru kushika silaha. Au angaliweza kukaza fikira juu ya farasi zake zenye kutimua mbio zikashambulie, huku mwandamani fulani akizitumia silaha. Magari-vita hayo yalikuwa na miundu ya chuma yenye kunyooka kutoka kwenye vikombe vya magurudumu. Ni lazima magari-vita hayo yaliyotungama pamoja yawe yaliogopesha wanaume wa Baraki wenye ku-tazama chini wakiwa kwenye Tabori kwa kuyaona kana kwamba hayazuiliki wala kushindika.
Hata hivyo, Yehova alikuwa amemwahidi Baraka hivi: “Nami nitakuvutia Sisera . . . hata mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake.” Katika wakati ufaao, wale Waisraeli hodari walimiminika chini kwa kuteremkia ukingo wa Tabori.—Waamuzi 4:1-14.
Uliokuwa wa maana kuliko ile faida tu ya mtokeo wao wa ghafula ni msaada ambao Israeli walipokea kutoka kwa Mungu wao mwenye nguvu nyingi mbinguni. Baadaye Debora aliimba hivi: “Kutoka mbinguni nyota zilipigana, kutoka kwenye mizungukio yazo zilipigana dhidi ya Sisera. Bubujiko la Kishoni liliwaoshea mbali . . . Wewe ulienda ukikanyaga imara chini, O nafsi yangu.” (Waamuzi 5:20, 21, NW) Ndiyo, ingawa Waisraeli wenye silaha haba lakini wenye ushujaa walikimbiza Wakanaani, Mungu ndiye aliamua tokeo halisi. Alisababisha bubujiko la ghafula lenye kulemea liwe katika sakafu ya mto, likikwamisha magari-vita yale ya kuogopesha sana.
Hapa chini waona sehemu ya mto Kishoni. Katika majira yenye mvua, huo waweza kufurisha kingo zao na kugeuza eneo hilo liwe utopetope. Piga picha uwazie magari-vita ya Kikanaani yakijaribu kuponyoka kupitia matope ya jinsi hiyo. Yale maji yenye kupita kwa fujo yalichukua baadhi ya askari au magari-vita yenye kukimbia, au vyote viwili. Ushindi wa Israeli hata ulimfikia Jemadari Sisera, aliyekuwa ameachilia mbali gari-vita lake, akiponyoka kwa miguu kutoka ile mandhari ya pigano. Baada ya yeye kufanya kimbilio katika hema la mwanamke Yaeli, alichagua wakati ufaao sana akamwua adui huyo.—Waamuzi 4:17-22.
Hivyo, sura muhimu na ya ushindi wenye shangwe ilifunguka katika historia ya Israeli mbele ya Debora na wengine wowote ambao wangaliweza kuwa wakitazama wakiwa mahali pa wazi juu ya Mlima Tabori.
[Maelezo ya Chini]
a Ona ramani na foto ile kubwa iliyobainika wazi ya Tabori katika 1990 Calendar of Jehovah’s Witnesses.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 16]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 17]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.