-
‘Vita Ni vya Yehova’Mnara wa Mlinzi—1989 | Januari 1
-
-
1, 2. (a) Ni wito gani wa ushindani unaokabili jeshi la Israeli likiwa chini ya amri ya Mfalme Sauli? (b) Wanaume wa jeshi la Israeli wanaitikiaje wito wa ushindani wa Goliathi, na sasa ni nani anayetokea katika tamasha ile?
MAJESHI mawili yenye uweza yakabiliana ng’ambo-ng’ambo ya bonde la Ela, kusini-magharibi mwa Yerusalemu. Upande mmoja liko jeshi la Israeli, likiongozwa na Mfalme Sauli aliyewekwa katika cheo hivi karibuni. Upande ule mwingine liko jeshi la Wafilisti lenye bingwa wao aliye pandikizi la mtu, Goliathi. Inaelekea kwamba jina Goliathi linamaanisha “Mwenye Kutokea Wazi Sana.” Yeye ana urefu wa kama meta 2.7 na silaha zimemjaa tele. Goliathi anawapaazia Israeli sauti ya ukaidi wenye makufuru. —1 Samweli 17:1-11.
-
-
‘Vita Ni vya Yehova’Mnara wa Mlinzi—1989 | Januari 1
-
-
3. Daudi anajitayarishaje kwa vifaa vya vita, lakini Goliathi ana vifaa vya jinsi gani?
3 Anapomsikia Goliathi ‘akiwatukana majeshi ya Mungu aliye hai,’ Daudi anajitolea akapigane na jitu lile. Sauli anapotoa idhini, Daudi anachomosha mwendo lakini bila yale mavazi ya kidesturi wala silaha alizopewa na Sauli. Kifaa alicho nacho ni fimbo ya uchungaji, kombeo, na mawe matano tu yaliyo laini—tofauti na Goliathi, ambaye amechukua mkuki wenye kichwa cha kilogramu 7 na aliyevaa kinga ya koti lenye mabamba ya shaba la kilogramu 57! Huku Goliathi mwenye uweza na mchukuangao wake wakiwa wanasogea mbele, ‘Mfilisti huyo anamlaani Daudi kwa miungu yake.’—1 Samweli 17:12-44.
-