Israeli Katika Siku Za Daudi Na Sulemani
MUNGU aliahidi kuupatia uzao wa Abramu nchi ‘iliyotoka mto wa Misri mpaka mto Efrati.’ (Mwa 15:18; Kut 23:31; Kum 1:7, 8; 11:24) Baada ya Yoshua kuingia Kanaani, ilichukua muda wa karne nne hivi kwa Nchi ya Ahadi kufikia mipaka hiyo.
Mfalme Daudi aliwashinda Waaramu waliotawala ufalme wa Soba ambao ulienea hadi Mto Efrati kaskazini mwa Siria.a Daudi alipowashinda Wafilisti, alipanua miliki yake upande wa kusini hadi kufikia mpaka wa Misri.—2Sa 8:3; 1Nya 18:1-3; 20:4-8; 2Nya 9:26.
Naye Sulemani alitawala “kutoka ule Mto [Efrati] hadi kwenye nchi ya Wafilisti na hadi kwenye mpaka wa Misri.” Utawala wake ulifananisha utawala wenye amani wa Mesiya. (1Fa 4:21-25; 8:65; 1Nya 13:5; Zb 72:8; Zek 9:10) Hata hivyo, inasemekana kwamba eneo lililokaliwa na Waisraeli ‘lilianzia Dani mpaka Beer-sheba.’—2Sa 3:10; 2Nya 30:5.
Mfalme Sulemani alikosa kumtii Mungu alipojirundikia farasi na magari ya vita. (Kum 17:16; 2Nya 9:25) Angeweza kuendesha farasi na magari hayo kwenye mfumo wa barabara uliokuwako. (Yos 2:22; 1Fa 11:29; Isa 7:3; Mt 8:28) Ni barabara chache sana tunazoelezewa mahali zilipopitia. Kwa mfano, tunaelezwa kuhusu “njia kuu inayopanda kutoka Betheli kwenda Shekemu na kuelekea upande wa kusini wa Lebona.”—Amu 5:6; 21:19.
Kitabu The Roads and Highways of Ancient Israel kinasema: ‘Ni vigumu kuchunguza mfumo wa barabara uliokuwako katika Israeli la kale, kwa kuwa barabara zilizokuwako wakati wa Agano la Kale hazikuwekwa lami hivyo hazingedumu.’ Hata hivyo, sura ya nchi na magofu ya majiji yaliyofukuliwa yanaonyesha mahali barabara nyingi zilipopitia.
Mara nyingi barabara ziliwasaidia wanajeshi kuamua mahali ambapo wangeelekea. (1Sa 13:17, 18; 2Fa 3:5-8) Ili kushambulia Israeli, Wafilisti walipiga mwendo kutoka Ekroni na Gathi hadi kwenye eneo lililokuwa “kati ya Soko na Azeka.” Jeshi la Sauli lilikutana nao huko “katika nchi tambarare ya chini ya Ela.” Baada ya Daudi kumuua Goliathi, Wafilisti walikimbia na kurudi Gathi na Ekroni, naye Daudi akakwea Yerusalemu.—1Sa 17:1-54.
Lakishi (D10), Azeka (D9), na Beth-shemeshi (D9) zilikuwa kwenye njia iliyopitia Shefela kuelekea vilima vya Yudea. Kwa hiyo majiji hayo yalikuwa muhimu sana katika kuzuia maadui wasipitie njia ya Via Maris na kufika katikati mwa nchi ya Israeli.—1Sa 6:9, 12; 2Fa 18:13-17.
[Maelezo ya Chini]
a Eneo la wana wa Rubeni lilifika kwenye Jangwa la Siria, na mpaka wake wa mashariki ulifika Mto Efrati.—1Nya 5:9, 10.
[Sanduku katika ukurasa wa 16]
VITABU VYA BIBLIA TANGU WAKATI HUO:
Samweli wa 1 na 2
Zaburi (sehemu)
Methali (sehemu)
Wimbo wa Sulemani
Mhubiri
[Ramani katika ukurasa wa 17]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Maeneo Na Barabara Wakati Wa Ufalme Ulioungana
Mipaka (Wakati wa Sulimani)
Tifsa
Hamathi
Tadmori
Berothai (Kuni?)
Sidoni
Damasko
Tiro
Dani
Yerusalemu
Gaza
Aroeri
Beer-sheba
Tamari
Esion-geberi
Elathi (Elothi)
[Mito na Vijito]
Efrati
B.M. la Misri
Daudi na Sulemani (barabara)
B10 Gaza
C8 Yopa
C9 Ashdodi
C10 Ashkeloni
C11 Siklagi
C12 NYIKA YA PARANI
D5 Dori
D6 Heferi
D8 Afeki
D8 Rama
D9 Shaalbimu
D9 Gezeri
D9 Makazi
D9 Ekroni
D9 Beth-shemeshi
D9 Gathi
D9 Azeka
D10 Soko
D10 Adulamu
D10 Keila
D10 Lakishi
D11 Yatiri
D12 Beer-sheba
E2 Tiro
E4 Kabuli
E5 Yokneamu (Yokmeamu?)
E5 Megido
E6 Taanaki
E6 Arubothi
E7 Pirathoni
E8 Lebona
E8 Sereda
E8 Betheli
E9 Beth-horoni ya Chini
E9 Beth-horoni ya Juu
E9 Geba
E9 Gibeoni
E9 Gibea
E9 Kiriath-yearimu
E9 Nobu
E9 Baal-perasimu
E9 Yerusalemu
E9 Bethlehemu
E10 Tekoa
E10 Hebroni
E11 Zifu
E11 Horeshi?
E11 Karmeli
E11 Maoni
E11 Eshtemoa
F5 En-dori
F5 Shunemu
F5 Yezreeli
F6 Beth-sheani
F7 Tirsa
F7 Shekemu
F8 Sarethani
F8 Shilo
F8 Ofra?
F9 Yeriko
F11 En-gedi
G2 Abel-beth-maaka
G2 Dani
G3 Hasori
G3 MAAKA
G5 Lo-debari (Debiri)
G5 Rogelimu
G6 Abel-mehola
G7 Sukothi
G7 Mahanaimu
H1 SIRIA
H4 GESHURI
H6 Ramoth-gileadi
H8 Raba
H9 Medeba
H11 Aroeri
H12 MOABU
I4 Helamu?
I9 AMONI
[Babara kuu]
C10 Via Maris
H6 Barabara ya Mfalme
[Milima]
F5 Ml. Gilboa
[Bahari]
C8 Bahari ya Mediterania (Bahari Kuu)
F10 Bahari ya Chumvi
G4 Bahari ya Galilaya
[Chemchemi au kisima]
E9 En-rogeli
[Picha katika ukurasa wa 16]
Kulia: Bonde la Ela, vilima vya Yuda vikiwa upande wa mashariki
Chini: Barabara zilirahisisha usafiri katika Nchi ya Ahadi