-
Ninapaswa Kutoa Kiasi Gani cha Pesa?Mnara wa Mlinzi—2009 | Agosti 1
-
-
Nyakati nyingine, Waisraeli walitoa michango mingi au michache ya hiari kadiri walivyotaka. Kwa mfano, Mfalme Daudi alipopanga kumjengea Yehova hekalu, raia wake walitoa “dhahabu yenye thamani ya talanta elfu tano.”a (1 Mambo ya Nyakati 29:7) Tofautisha hilo na yale ambayo Yesu aliona alipokuwa duniani. Alimwona “mjane fulani mwenye uhitaji akitumbukiza . . . sarafu ndogo mbili za thamani ndogo sana” ndani ya sanduku la hazina la hekalu. Mchango wake ulikuwa wa kiasi gani? Ulikuwa tu 1/64 ya mshahara wa siku moja. Hata hivyo, Yesu alisema kwamba kiasi hicho kidogo kilikubalika.—Luka 21:1-4.
-
-
Ninapaswa Kutoa Kiasi Gani cha Pesa?Mnara wa Mlinzi—2009 | Agosti 1
-
-
a Katika mwaka wa 2008, bei ya wastani ya dhahabu ilikuwa dola 871 za Marekani kwa wakia au gramu 28.35, hivyo mchango huo ulikuwa na thamani ya dola 4,794,855,000 za Marekani.
-