-
Aliwatetea Watu wa MunguIgeni Imani Yao
-
-
22. Kwa nini Esta aliogopa kwenda mbele ya mume wake aliyekuwa mfalme? (Ona pia maelezo ya chini.)
22 Bila shaka, Esta alihangaishwa na ujumbe huo. Lilikuwa jaribu kali sana la imani yake. Aliogopa na jambo hilo lilionekana wazi katika jibu lake kwa Mordekai. Alimkumbusha kuhusu sheria ya mfalme. Ikiwa angeenda mbele ya mfalme bila kuitwa, angeuawa. Lakini hangeuawa kama mfalme angemnyooshea fimbo yake ya dhahabu. Je, Esta alikuwa na sababu yoyote ya kutazamia kwamba hangeuawa, hasa akikumbuka kilichompata Vashti alipokataa kwenda mbele ya mfalme alipoagizwa kufanya hivyo? Alimwambia Mordekai kwamba mfalme hakuwa amemwita kwa siku 30! Hivyo, Esta hakujua ikiwa alikuwa amepoteza kibali cha mfalme ambaye hisia zake zilibadilika-badilika.e—Esta 4:9-11.
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguIgeni Imani Yao
-
-
e Shasta wa Kwanza alikuwa mkatili na mwenye hisia zilizobadilika-badilika. Mwanahistoria Mgiriki, Herodoto, aliandika mambo fulani kuhusu vita kati ya Shasta na Wagiriki. Mfalme aliagiza daraja la meli lijengwe kwenye mlango wa bahari wa Hellespont. Dhoruba ilipofagilia mbali daraja hilo, Shasta aliagiza mafundi wake wakatwe vichwa na watu wake “waadhibu” Hellespont kwa kupiga maji huku ujumbe wa matusi ukisomwa kwa sauti kubwa. Wakati wa vita hivyo, tajiri fulani alipoomba mwanawe asijiunge na jeshi, Shasta aliagiza kijana huyo akatwe vipande viwili na mwili wake uwekwe mahali palipo wazi ili kuwa onyo kwa wengine.
-