-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Bila shaka, Esta aliingiwa na wasiwasi alipopata ujumbe huo. Lilikuwa jaribu kubwa sana la imani yake. Aliogopa na jambo hilo lilionekana wazi katika jibu lake kwa Mordekai. Esta alimkumbusha sheria ya mfalme. Ikiwa angeenda mbele ya mfalme bila kuitwa, angeuawa. Lakini mtu hangeuawa ikiwa mfalme angemnyooshea fimbo yake ya enzi ya dhahabu. Je, Esta alikuwa na sababu yoyote ya kutazamia kwamba hangeuawa, hasa akikumbuka kilichompata Vashti alipokataa kwenda mbele ya mfalme alipoagizwa kufanya hivyo? Alimwambia Mordekai kwamba mfalme hakuwa amemwita kwenda mbele yake kwa siku 30! Kwa sababu hakuwa ameitwa kwa siku nyingi, Esta hakujua ikiwa alikuwa amepoteza kibali cha mfalme ambaye hisia zake zilibadilika-badilika.d—Esta 4:9-11.
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
d Shasta wa Kwanza alikuwa na hisia zilizobadilika-badilika na hasira yenye jeuri. Herodoto, mwanahistoria Mgiriki, aliandika mambo fulani ambayo Shasta alifanya wakati wa vita vyake na Wagiriki yanayoonyesha hisia za mfalme huyo. Mfalme aliagiza daraja la muda la meli zilizounganishwa lijengwe ili kuvuka mlango wa bahari wa Hellespont. Dhoruba ilipofagilia mbali daraja hilo, Shasta aliagiza mafundi wake wakatwe vichwa na watu wake “waadhibu” Hellespont kwa kupiga maji huku ujumbe wa matusi ukisomwa kwa sauti kubwa. Pindi hiyo, mwanamume fulani tajiri alipoomba mwana wake asiandikishwe jeshini, Shasta aliagiza kijana huyo akatwe vipande viwili na mwili wake uwekwe mahali palipo wazi ili kuwa onyo kwa wengine.
-