“Hofuni Mungu na Kumpa Yeye Utukufu”
“Hofuni Mungu na kumpa yeye utukufu.”—UFUNUO 14:7, NW.
1. Inatupasa sisi kuhofu nani, na haitupasi sisi kuhofu nini?
INATUPASA SISI KUMHOFU NANI? Kwa hakika si yule drakoni mwenye rangi-moto, Shetani, na jeshi lake la roho waovu! Kristo Yesu alivurumisha hao nje ya mbingu kufuatia uzaliwa wa Ufalme katika 1914. Lakini ndipo njozi za Apokalipsi zinapofunua tengenezo ambalo Shetani anatumia hapa duniani katika jitihada yake ya kufa na kupona ya kuzuia makusudi ya Mungu. Wenye kutokeza katika wonyesho huu wa picha ni hayawani wawili wakali na malaya mlevi—Babuloni Mkuu. Je! inatupasa sisi kuwahofu hawa? Mbali sana na hilo! Badala ya hilo, inatupasa sisi kuhofu Yehova na Kristo wake, ambaye Ufalme wake umeleta ulimwengu mfisadi wa Shetani kwenye hukumu yao ya tamati.—Mithali 1:7; Mathayo 10:28; Ufunuo 12:9-12.
Hayawani Wenye Kukufuru
2. Ni hayawani-mwitu yupi anayetokea aonekane katika njozi ya nane, na anawakilisha nini?
2 Ile njozi ya nane ya Ufunuo ifungukapo, hayawani-mwitu anainuka kutoka bahari yenye msukosuko ya aina ya binadamu. Ana vichwa saba na pembe kumi pamoja na mataji kumi, kuashiria mamlaka ya kifalme aliyopewa na Shetani. Anakufuru Yehova, akiwaumiza vibaya watumishi Wake kama ambavyo chui, dubu, au simba angefanya; lakini mamlaka yake ni ya kitambo tu, ikiwa imetoka kwa yule drakoni, Shetani, ambaye anafanana naye sana. Mapema zaidi mnabii Danieli alikuwa ameeleza serikali za kisiasa za kidunia kuwa hayawani, na serikali zenyewe mara nyingi huchagua viumbe wa mwituni kuwa ishara zao za kitaifa, kama vile simba wa Uingereza na tai wa Amerika. (Danieli 8:5-8, 20-22) Ingawa hivyo, sasa sisi twaona hayawani wa muungano, ambaye ni kutia ndani serikali zote za kisiasa za historia ya Biblia ambazo mara nyingi sana zimekandamiza watumishi wa kweli wa Mungu duniani. “Vichwa” vyenye kutokeza miongoni mwa hivyo vimekuwa Misri, Ashuri, Babuloni, Umedi-Uajemi, Ugiriki, Roma, na mwishowe ile Serikali Kubwa ya Uwili ya Uingereza-Amerika.—Ufunuo 13:1, 2; 12:3, 7-9.
3. (a) Kimoja cha vichwa vya hayawani-mwitu kilipokeaje “pigo la upanga”? (b) Hayawani-mwitu mwenye pembe mbili anachukuaje uongozi katika kufanyiza mfano wa hayawani-mwitu wa kwanza? (c) Ni nini jina la hayawani-mwitu wa kwanza na jina hilo lina maana gani?
3 Wakati wa vita ya ulimwengu ya 1914-18, Uingereza, ikiwa serikali ya saba ya ulimwengu, ilipokea “pigo la upanga” ambalo lingeleta kifo. Lakini United States ya Amerika ikaja kuiponyoa. Tangu hapo, Amerika na Uingereza zimeshirikiana zikiwa serikali kubwa ya ulimwengu ya uwili, ambayo Yohana huendelea kusimulia kuwa hayawani-mwitu mwenye pembe mbili, anayetoka kwa jamii ya kibinadamu iliyosimamishwa imara, “dunia.” Hayawani-mwitu huyu huchukua uongozi katika kufanyiza mfano wa yule hayawani wa kwanza na kuvuvia uhai ndani yao, kutaswiri jinsi Serikali Kubwa ya Uingereza na Amerika ilivyokuja kuwa mdhamini mkuu na mpaji uhai kwa ule Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao, Umoja wa Mataifa. Hayawani-mwitu wa kwanza ana jina-nambari, 666. Sita ni nambari isiyokamilika—ikipungukia saba ambayo ni nambari kamilifu ya Kibiblia—hivi kwamba sita kwa kiwango cha tatu hudokeza kutokamilika kubaya sana kwa utawala wa kibinadamu leo. Ingawa Mashahidi wa Yehova huheshimu serikali na wao ni mfano mzuri katika kutii sheria za bara wanamoishi, wao wanakataa kwa ujasiri kuabudu “hayawani-mwitu” au mfano wake.—Ufunuo 13:3-18, NW; Warumi 13:1-7.
Hofu Mungu—Kwa Nini?
4. (a) Ni nani wanaonwa wakisimama juu ya Mlima Sayuni wa kimbingu, na wale wazee 24 walio mbele ya kiti cha ufalme cha Mungu ni picha ya nani? (b) Tofauti ni nini kati ya “wimbo mpya” unaoimbwa na wapakwa-mafuta na “wimbo mpya” unaoimbwa na umati mkubwa?
4 Kwa wakati uliopo, mambo ya hayawani hayo yametosha! Kwa tofauti yenye kuburudisha, njozi ya tisa hulenga juu ya Mwana-Kondoo. Yeye anasimama juu ya Mlima Sayuni, pamoja na wale 144,000 ambao yeye hununua wakiwa matunda ya kwanza kutoka miongoni mwa aina ya binadamu. Ingawa baadhi ya hao wangali wanatumikia duniani, katika maana ya kiroho wote 144,000 ‘wamekaribia Mlima Sayuni na . . . Yerusalemu la kimbingu.’ (Waebrania 12:22, NW) Kwa kufaa, wale wazee 24 wanaonwa hapa pia mbele ya kiti cha ufalme cha Mungu, kwa kuwa wao ni picha ya kikundi kile kile kilichopakwa mafuta kikionwa kutoka kituo-msimamo kilicho tofauti—kama kimekwisha fufuliwa na kuwekwa kuwa wafalme na makuhani. Hao 144,000 wanaimba “wimbo mpya.” Huo unatokana na tukio lisilo na kifani la kununuliwa kwao kutoka katika dunia ili wawe warithi wa Ufalme. Umati mkubwa pia ‘waimbia Yehova wimbo mpya,’ lakini huo ni tofauti katika maana ya kwamba wanaimba kwa kutarajia kufikia uhai wa milele katika milki ya kidunia ya Ufalme.—Ufunuo 7:9; 14:1-5; Zaburi 96:1-10; Mathayo 25:31-34, NW.
5. (a) Ni habari zipi zinazotangazwa na malaika anayeruka katikati ya mbingu, na kwa nini ni za milele? (b) Malaika huyo anatoa amri gani kwa sauti kuu, na kwa nini hii inafaa sana?
5 Njozi hiyo sasa yapanuka. Yohana aona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu. Na habari za kutangaza alizo nazo ni za kuteremesha kama nini! Ni habari njema za milele, kwa kuwa humaanisha uhai wa milele kwa wale wa kutoka katika kila taifa na kabila na ulimi na kikundi cha watu ambao hutii Mungu katika saa hii ya hukumu. Kwa kutofautiana na hayawani wenye kuchukiza ambao Yohana ametoka kuelezea sasa tu, kwa nini Mungu huyu asipaswe kuabudiwa, ndiyo, kusifiwa? Yeye ndiye Mmoja ambaye aliumba mbingu na dunia. Yeye ndiye Chanzo cha kila kitu kilichopo, kilicho na uhai na kisicho na uhai. Kuna sababu imara, basi, kwa huyo malaika kuamuru kwa sauti zenye mamlaka: “HOFUNI MUNGU NA KUMPA YEYE”! Sauti ya malaika huyu inasikiwa kuzunguka dunia yote, na katika lugha zapata 200 Mashahidi wa Yehova hurudisha mwangwi wa mwaliko wake unaoamsha aina ya binadamu yote.—Ufunuo 14:6, 7, NW; Isaya 45:11, 12, 18.
Anguko la Babuloni Mkuu
6. Ni habari gani zenye kugutusha anazotangaza malaika mwingine?
6 Malaika mwingine atokea. Ujumbe atangazao ni wenye kugutusha kweli kweli: “Yeye ameanguka! Babuloni Mkuu ameanguka, yeye ambaye alifanya mataifa yote kunywa ya divai ya kasirani ya uasherati wake!” (Ufunuo 14:8, NW) Babuloni Mkuu ni nani, hivi kwamba yeye anaweza kutongoza mataifa na kuyalevya?
7. Babuloni Mkuu ni nini, na alisitawije?
7 Babuloni la kale lilikuwa kibubujiko kikuu cha dini bandia, nacho kilipanuka kikaenea duniani pote kikawe milki ya ulimwengu ya roho waovu, ambayo kwa kufaa ilibandikwa jina “Babuloni Mkuu.” Baada ya wakati kupita, Roma likawa lenye kutokeza katika milki hiyo ya kidini, kwa maana ilikuwa ni chini ya Roma kwamba Ukristo wenye kuasi imani ulisitawi. Roma laendelea kuwa kitovu cha dini ya Kibabuloni. Jambo hilo lilionekana wazi katika 1986 wakati viongozi wa kidini wa ulimwengu walipoitikia wito wa papa wa Roma kwa kukusanyika pamoja na yeye katika Assisi, karibu na Roma, kusali kwa ajili ya Mwaka wa Amani ya Kimataifa uliotangazwa na Umoja wa Mataifa.
8. (a) Babuloni Mkuu alipatwaje na anguko kubwa, na ithibati ya jambo hilo inaonekana tangu lini? (b) Ni nini linaloonyesha kwamba sala za viongozi wa kidini kwa ajili ya amani huenda bila kujibiwa?
8 Hata hivyo, Babuloni Mkuu amepatwa na anguko kubwa! Ithibati ya jambo hilo imekuwa wazi tangu 1919 katika upungufu wa kuungwa mkono kwa dini bandia ulimwenguni pote. Ukomunisti usioitikadi kuwako kwa Mungu sasa hudhibiti maeneo makubwa ya dunia. Vijana wa leo wanafundishwa mageuzi, ambayo hupinganisha Neno la Mungu. Katika Ulaya ya Kiprotestanti watu ambao wangali wakihudhuria kanisa ni wachache, na papa mwenye kusafiri-safiri anajitahidi sana kuungamanisha milki yake ya Kikatoliki. Kwa wazi sala kwa miungu mingi ya dini za ulimwengu huenda bila kujibiwa. Ruth L. Sivard aliripoti: “Vita ishirini na viwili vilikuwa vikiendelea katika 1987, vita vingi zaidi kuliko mwaka wowote uliotangulia katika historia iliyorekodiwa. Jumla ya vifo katika vita hivi kufikia sasa ni angalau 2,200,000—na vinaongezeka kasi.”a Lo! jinsi mkutano wa sala Assisi ulivyothibitika kukosa matokeo! Na bado katika 1987 papa aliutia alama ukumbusho wa mwaka wa kwanza wa kusanyiko hilo kwa kutokeza sarafu yenye sura yake upande mmoja na ishara ya mkutano huo wa sala upande ule mwingine. Wao hufuliza “kusema, ‘Kuna amani! Kuna amani!’ wakati hakuna amani.”—Yeremia 6:14, NW.
Ukahaba wa Babuloni Wafunuliwa
9. Viongozi wa kidini wa Babuloni Mkuu wamekuwa na sifa mbaya kwa njia zipi za ukosefu wa adili?
9 Ufunuo 14:8 huonyesha kwamba Babuloni Mkuu ni mwasherati wa kike. Viongozi wa kidini wake wamekuwa wenye sifa mbaya kwa njia zao za ukosefu wa adili. Waevanjeli wa TV wamenyoa makundi yao mamia ya mamilioni ya dola, huku wakati ule ule wakifanya ukosefu wa adili wenye aibu. Upadri wa Kikatoliki pia ni wenye kutilika mashaka sana, kama inavyoonyeshwa na ripoti inayofuata katika The Beacon Journal la Philadelphia, Pennsylvania, Januari 3, 1988: “Mamia ya watoto walioshikwa-shikwa uchi wao na mapadri Wakatoliki katika United States katika pindi ya miaka mitano iliyopita wametaabishwa na maumivu makali ya kimoyoni, wasema wazazi, wasaikolojia, maofisa wa polisi na mawakili waliohusika katika kesi hizo.” Ukosefu wa adili katika ngono umeleta sifa mbaya juu ya wengi wa viongozi wa kidini wa Babuloni Mkuu.
10. (a) Kwenye Ufunuo 18:3, ni nini linaloonyeshwa na “uasherati” wa Babuloni Mkuu? (b) Kama inavyoonyeshwa kwenye Ufunuo 18:24, kwa nini viongozi wa kidini wa Babuloni Mkuu wanashiriki hatia kubwa ya umwagaji-damu?
10 Ingawa hivyo, “ile divai ya kasirani ya uasherati wake” inarejezea hasa ubembelezi wa dini bandia kwa watawala, kuunga mkono kampeni za kisiasa na vita vyao, na kushurutisha watu waabudu kisehemu fulani cha utukuzo wa taifa cha yule hayawani-mwitu. Mara nyingi wanasiasa wamepata dini ikiwa mwenzi mwenye mafaa katika kujipatia wanayotaka, kama inavyoweza kuonwa katika mapatano ya Hitler na Vatikani katika 1933 na ile Vita ya Wenyeji ya Kihispania ya 1936-39. Wakati wa Vita ya Ulimwengu 2, viongozi wa dini ya Ukatoliki, Uprotestanti, Ubudha, na dini nyinginezo katika pande zote mbili walitenda kana kwamba walikuwa wamelevywa na harara ya vita. Wao wanashiriki hatia kubwa ya damu ya makumi ya mamilioni ya askari-jeshi na raia ambao wamekufa katika vita tangu 1914. Viongozi wa kidini waliounga mkono Wafashisti na Wanazi wana hatia ya damu pia kwa sababu ya Mashahidi wa Yehova, na wengine, ambao walifishwa kwa amri ya serikali au waliokufa katika kambi za mateso.—Yeremia 2:34; Ufunuo 18:3, 24.
11. (a) Wakristo wapakwa-mafuta na umati mkubwa wamekataa kuabudu nini? (b) Ni mataraja gani mazuri sana yanayotoa sababu yenye nguvu nyingi ya kuhofu Mungu na kumpa yeye utukufu?
11 Wakati wa miaka 74 iliyopita, Wakristo washikamanifu wapakwa-mafuta, pamoja na nambari zenye kuongezeka za umati mkubwa, wameendelea KUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU. Sisi tumekataa kwa imara kuabudu kisehemu chochote cha hayawani-mwitu cha utukuzo wa taifa. Sisi tumekataa kutukuza ule mfano wa hayawani—Ushirika wa Mataifa na UM—kwa kuwa sisi tunang’amua kwamba ni “ufalme wa Bwana [Yehova] wetu na wa Kristo wake” tu unaoweza kuleta amani na usalama wa kweli. Sisi tumepiga moyo konde tushike “amri za Mungu na imani ya Yesu.” Uvumilivu huo una thawabu! Wakristo wapakwa-mafuta ambao “hufa katika muungano pamoja na Bwana” wamehesabiwa kuwa wenye furaha, kwa kuwa “vitu walivyofanya huenda moja kwa moja pamoja nao.” Kwa habari ya wowote wa mkutano mkubwa ambao huenda wakafa chini ya minyanyaso, kutokana na ugonjwa, au kwa aksidenti, urafiki ambao wamesitawisha pamoja na Mungu huwahakikishia ufufuo wa mapema kuingia ndani ya jamii ya “dunia mpya.” Mataraja haya matukufu hutoa sababu zenye nguvu kweli kweli za KUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU.—Ufunuo 11:15, 17; 12:10; 14:9-13; 21:1, NW.
12. Ni mavuno gani mawili yanayotukia, na wakati gani?
12 Hukumu iendeleapo, malaika wanatoa wito kuwe na mavuno mawili. Ni wazi kwamba mvunaji wa kwanza ni Yesu, aliyeketishwa juu ya kiti cha ufalme katika utukufu wa Ufalme tangu 1914, kwa kuwa yeye ameketi juu ya wingu jeupe, amevikwa taji, na ni “kama mwana wa binadamu.” Sasa, katika siku ya Bwana, yeye anavuna dunia, kwanza wale wabakio wa Wakristo wapakwa-mafuta, kisha mamilioni ya umati mkubwa. (Linganisha Mathayo 25:31-34; Yohana 15:1, 5, 16.) Kwa kutofautisha, vuno la pili ni lile la “mzabibu wa dunia” ambalo linatupwa ndani ya “shinikizo kubwa la divai ya kasirani ya Mungu.” Hii ndiyo hukumu inayofikilizwa kwenye Har–Magedoni, wakati jamii ya kibinadamu iliyo mbovu na yenye mvurugo inapong’olewa, na tunda layo lenye sumu linapondwa-pondwa kuwa teketeke. Yehova na atukuzwe kwa kuiondolea dunia mzabibu huu wenye sumu!—Ufunuo 14.14-20; 16:14, 16, NW.
“Yehova . . . Mwadilifu na wa Kweli”
13. (a) Katika njozi ya kumi, ni wimbo gani wanaoimba wapakwa-mafuta waliofufuliwa, na wimbo huo una maneno gani? (b) Hukumu za Mungu za uadilifu zinaonyeshwaje waziwazi katika njozi hii?
13 Katika njozi ya kumi ya Ufunuo, sisi tunaona tena matukio ya kimbingu mbele ya kiti cha ufalme cha Mungu. Ni mshangilio ulioje unaoambatana na kuwapo kwake! Wapakwa-mafuta waliofufuliwa—walioshinda kwa sababu ya KUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU—wanaimba ‘wimbo wa Musa na wa Mwana-Kondoo’: “Kubwa na za ajabu ni kazi zako, Yehova Mungu, yule Mweza Yote. Za uadilifu na za kweli ni njia zako, Mfalme wa umilele. Ni nani ambaye kwa kweli hatahofu wewe, Yehova, na kutukuza jina lako, kwa sababu wewe pekee ni mshikamanifu? Kwa maana mataifa yote yatakuja na kuabudu mbele zako wewe, kwa sababu amri zako za uadilifu zimefanywa zidhihirike.” Hukumu za Mungu ni za uadilifu kweli kweli na za kweli, kama ambavyo imeonyeshwa kwa wazi katika njozi hii yote! Malaika wamwaga mabakuli saba ya kasirani ya Mungu, hiyo ikitokeza mkusanyo wa mataifa yote kwenye Har–Magedoni na kikumbusho cha kwamba “Babuloni Mkuu alikumbukwa katika mwono wa Mungu”! Wito wa KUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU ni wa wakati unaofaa kweli kweli.—Ufunuo 15:1–16:21, NW.
14. Katika njozi ya 11 na 12, Babuloni mkuu anakuwa na sehemu gani yenye kutokeza, na kwa nini huu ndio wakati wa kumwacha mara moja?
14 Babuloni Mkuu anatajwa mara kwa mara katika Ufunuo. Sisi twamuona tena akiwa umbo lenye kutokeza katika njozi ya 11 na 12. Yeye “anaketi juu ya maji mengi,” akidhibiti vikundi vya watu na kuwafanya walevywe na mafundisho yake bandia ya kidini, yenye sumu. Yeye mwenyewe amelevywa na “damu ya wale watakatifu,” ambao amewaua kwa minyanyaso, na yeye ni mwenye hatia ya damu kwa habari ya “wote ambao wamechinjwa juu ya dunia,” kwa sababu ya yeye kuchochea vita kwa hila. Uenzi wake wa kuendesha shughuli pamoja na biashara kubwa na kukamua watu fedha umemletea utajiri mwingi uliopatikana isivyo haki. Lawama yake yenye kutokeza zaidi imekuwa kucheza-cheza kwake katika mahaba ya kisiasa, hata kufikia kufanya hila ajipatie umashuhuri kwa kumpanda hayawani wa amani—UM. Lakini utawadia wakati ambapo pembe zilizopewa kani za kijeshi za hayawani huyo huyo zitamrarua vipande vipande na kumharibu. Kwa wote ambao HUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU huu ndio wakati wa kumwacha huyo, “kwa kuwa madhambi yake yametungamana pamoja mpaka kwenye mbingu, na Mungu ameita matendo yake ya utovu wa haki kwenye akili.”—Ufunuo 17:1-18:24, NW.
15. Uharibifu wa kahaba mkuu huongoza kwenye wimbo gani wa sifa na unafuatwa na tukio gani jingine la furaha?
15 Kwa hiyo, kufishwa kwa Babuloni Mkuu huja ikiwa ni hukumu ya uadilifu kutoka kwa Yehova. Kwa kuthamini jambo hilo, ‘Haleluya’ zasikika, katika mbingu na kisha duniani, zikimhesabia Yehova wokovu, utukufu, na uweza. Korasi hizi za “Sifuni Yah, nyinyi watu!” huonyesha shangwe kubwa juu ya uharibifu wa milele wa huyo kahaba mkuu. Lo! mteketezo wake unatofautiana kama nini na tukio lenye furaha sana katika mbingu—ndoa ya Mwana-Kondoo, Kristo Yesu na bibi-arusi wake, wale washindi waaminifu 144,000! Wimbo wa sifa wenye kishindo wainuliwa kwa “Yehova Mungu wetu, yule Mweza Yote,” ndiyo, “acheni sisi tushangilie na tufurikwe na shangwe, na acheni sisi tumpe yeye utukufu, kwa sababu ndoa ya Mwana-Kondoo imefika na mke wake amejitayarisha mwenyewe”!—Ufunuo 19:1-10, NW.
16. Kulingana na njozi ya 13, ni suala gani litakalomalizwa mwishowe, na jinsi gani?
16 Hata hivyo, kabla haijatukia hiyo ndoa ya kimbingu, njozi ya 13 huonyesha jinsi suala linalohusu enzi kuu ya Yehova linavyomalizwa. Yesu, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana aliye wa Yehova, na majeshi ya malaika yakiandamana naye, “ahukumu na kuendeleza vita katika uadilifu,” akikanyaga shinikizo la divai ya kasirani ya hasira-kisasi ya Mungu Mweza Yote. Kila sehemu inayobaki ya mfumo wa Shetani inapondwa vipande vipande, inasagwasagwa! (Ufunuo 19:11-21, NW) Tunapoona kupitia njozi za Ufunuo ushindi huo wenye shangwe ukikaribia haraka sana, hakika sisi tuna kila sababu ya KUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU!
Kumtukuza Mungu kwa Umilele
17. Njozi ya 14 na 15 hufunua nini juu ya tokeo lenye furaha kwa wale wote ambao huhofu Mungu na kumpa yeye utukufu?
17 Njozi za 14 na 15 hufunua lile tokeo la furaha kwa wale ambao KUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU. Shetani na roho wake waovu wakiisha kutiwa ndani ya abiso kwa miaka elfu, ndoa ya kimbingu ya Mwana-Kondoo na bibi-arusi wake inatukia, na hawa wafalme na makuhani 144,001 wanatawala kwa miaka elfu wakiinua aina ya binadamu kwenye ukamilifu. Baada ya mtihani wa mwisho, wale ambao huendelea KUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU watashinda na kupata kibali cha uhai wa milele. Hao watakuwa ni kutia ndani mabilioni ya wafu wafufuliwa, “wale wakubwa na wale wadogo,” wenye kuthibitisha wanastahili kuandikisha majina yao katika kile kitabu cha uhai. “Mbingu mpya na dunia mpya” zitaletea aina ya binadamu baraka zisizoelezeka, baraka zilizohakikishwa, kwa maana Yehova akiwa Mfanyizaji wa “vitu vyote kuwa vipya,” atangaza hivi: “Andika, kwa sababu maneno haya ni yenye kuitibarika na ni ya kweli.”—Ufunuo 20:1–21:8, NW.
18. Kulingana na njozi ya 16, ni nini upeo wa kitabu cha Ufunuo?
18 Njozi ya 16 huleta upeo wa Ufunuo uonekane wazi. Huo ni nini? Ni njozi ya jiji. Jiji hili, Yerusalemu jipya, ni tofauti sana na lolote ambalo binadamu amepata kujenga hapa duniani—tofauti sana sana na Babuloni Mkuu, jiji ambalo uasi-imani walo, maadili machafu-machafu, na ukahaba wa kisiasa humwondolea sana Mungu heshima. Jiji hilo takatifu ni lenye kutakata, safi, lenye thamani kubwa. Ni bibi-arusi wa Mwana-Kondoo, mwenzi-msaidizi wake katika kutolea ulimwengu wa aina ya binadamu uhai wa milele. (Yohana 3:16) Si ajabu kwamba wito unavumishwa kwa sauti kuu na kwa wazi, wa kutoka katika hilo jiji bandia, Babuloni Mkuu!—Ufunuo 18:4; 21:9–22:5
19. (a) Ni mwaliko gani unaotolewa kupitia ile jamii ya bibi-arusi, na wasikivu wanaitikiaje? (b) Kutoa kwetu itikio chanya kwa ile amri ya “hofuni Mungu na kumpa yeye utukufu” kutatokeza nini?
19 Roho ya Yehova yenye nguvu-msukumo hutokeza kupitia jamii ya bibi-arusi mwaliko wenye kuhimiza: “Njoo!” Ndiyo, nyinyi nyote wasikivu ambao hutamani uhai wa milele katika paradiso ya tufe lote, njooni kwenye “mto wa maji ya uhai,” mkikubali maandalizi yote ya Yehova kupitia Kristo na bibi-arusi wake kwa ajili ya kupata uhai wa milele! Lo! hilo ni taraja zuri kama nini—uhai wa kibinadamu katika ukamilifu juu ya dunia paradiso! Hiyo itakuwa ndiyo thawabu kwa wale wengi wanaotoa jibu chanya kwa ile amri: “KUHOFU MUNGU NA KUMPA YEYE UTUKUFU”!—Ufunuo 22:6-21, NW.
[Maelezo ya Chini]
a World Military and Social Expenditures 1987-88.
WEWE UNGEJIBUJE?
◻ Kuna maagizo gani ya wakati unaofaa kwa ajili yetu katika njozi ya hayawani-mwitu wawili?
◻ Inatupasa sisi kuitikiaje tangazo la malaika anayeruka katikati ya mbingu?
◻ Babuloni Mkuu anahusikaje katika uasherati, na hilo linaonwaje na wale ambao huhofu Mungu?
◻ Dunia inavunwaje katika wakati wa siku ya Bwana?
◻ Ni matukio gani yenye furaha hufunga Ufunuo, na watu wa Mungu wanaweza kushirikije humo?
[Picha katika ukurasa wa 23]
Medali hii ya shaba ilitolewa katika Oktoba 1987 katika tarehe ya kukumbuka mwaka wa kwanza wa Sala kwa Ajili ya Amani huko Assisi. Kwenye upande mmoja kuna mfano wa “Baba Mtakatifu” ambaye amezungukwa na tarehe na maandishi haya: “John Paul II Pontifex Maximus.” Kwenye upande ule mwingine “Mtakatifu Francis” anatoa wito kuwe na “Amani ile Zawadi ya Mungu” kwenye Mkutano wa Assisi wa Sala kwa Ajili ya Amani