-
Je, Wengine Hulikubali Shauri Lako?Mnara wa Mlinzi—1999 | Januari 15
-
-
Unapotoa shauri, ni muhimu kuteua maneno yanayofaa. Solomoni, mtu mwenye hekima, alisema: ‘Neno linenwalo wakati wa kufaa, ni kama machungwa [“matofaa ya dhahabu,” NW] katika vyano vya fedha.’ (Mithali 25:11) Huenda Solomoni alifikiria chombo cha fedha kilichotiwa nakshi vizuri kikiwa na matofaa ya dhahabu yaliyochongwa vizuri sana juu yake. Chano hicho kingependeza jicho jinsi gani, nawe ungependezwa jinsi gani kukipokea kama zawadi! Kwa njia hiyohiyo, maneno yaliyoteuliwa vizuri, yapendezayo, yaweza kumvutia sana mtu unayejaribu kusaidia.—Mhubiri 12:9, 10.
-
-
Je, Wengine Hulikubali Shauri Lako?Mnara wa Mlinzi—1999 | Januari 15
-
-
Kama alivyosema Solomoni, neno la kushauri lapasa kunenwa “wakati wa kufaa.” Ili shauri lifanikiwe, ni muhimu litolewe wakati unaofaa! Ni wazi kwamba huenda mtu ambaye amepoteza hamu yake ya chakula asikithamini chakula. Labda amekula chakula kingi karibuni, au huenda yeye ni mgonjwa. Kumlazimisha mtu asiyetaka kula ale si jambo la hekima wala halikubaliki.
-