Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Heri Mtu Yule Aonaye Hekima”
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 15
    • “Anapiga Kelele”

      Sura ya 8 ya Mithali yaanza kwa swali lisilohitaji jibu: “Je! hekima halii? ufahamu hatoi sauti yake?”a Naam, hekima na ufahamu waendelea kulia, lakini kwa njia iliyo tofauti kabisa na mwanamke asiye na maadili anayeotea mahali penye giza na kumnong’onezea maneno ya utongozi kijana asiye na ujuzi. (Mithali 7:12) “Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.” (Mithali 8:1-3) Sauti kubwa na ya ujasiri ya hekima yasikika kwa nguvu na waziwazi mahali pa umma—malangoni, penye njia panda, mahali pa kuingia mjini. Watu wanaweza kusikia sauti hiyo kwa urahisi na kuitikia.

      Ni nani awezaye kukana kwamba karibu kila mtu duniani anaweza kupata hekima ya Mungu iliyo katika Neno lake lililopuliziwa, Biblia? “Biblia ni kitabu ambacho kimesomwa na watu wengi zaidi katika historia,” chasema kichapo The World Book Encyclopedia. Chaongezea hivi: “Biblia ndiyo imegawanywa kwa wingi zaidi kuliko kitabu kingine chochote. Biblia imetafsiriwa pia mara nyingi zaidi, na katika lugha nyingi zaidi, kuliko kitabu kingine chochote.” Kwa kuwa Biblia nzima au visehemu vyake vyapatikana katika lugha na lahaja zaidi ya 2,100, zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaweza kusoma angalau sehemu fulani ya Neno la Mungu katika lugha yao wenyewe.

      Mashahidi wa Yehova wanatangaza hadharani ujumbe wa Biblia kotekote. Katika nchi 235, wanahubiri kwa bidii habari njema za Ufalme wa Mungu na kufundisha watu kweli inayopatikana katika Neno la Mungu. Nakala zaidi ya milioni 20 hugawanywa za majarida yao yanayotegemea Biblia ambayo ni Mnara wa Mlinzi, jarida linalochapishwa katika lugha zaidi ya 140, na Amkeni! jarida linalochapishwa katika lugha 83. Bila shaka, hekima inaendelea kupiga kelele katika mahali pa umma!

  • “Heri Mtu Yule Aonaye Hekima”
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 15
    • a Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “hekima” liko katika ngeli ya kike. Kwa hiyo, watafsiri fulani hutumia viwakilishi vya ngeli ya kike wanaporejezea hekima.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki