-
Atimiza Unabii wa IsayaYesu—Njia, Kweli, na Uzima
-
-
“Tazama! Mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, ambaye nimemkubali! Nitaweka roho yangu juu yake, naye atayatangazia mataifa haki. Hatagombana wala kupiga kelele, wala yeyote hatasikia sauti yake kwenye barabara kuu. Hataponda tete lililovunjika, wala hatazima utambi unaofifia, hadi atakapofanikiwa kuleta haki. Kwa kweli, mataifa yatalitumainia jina lake.”—Mathayo 12:18-21; Isaya 42:1-4.
-
-
Atimiza Unabii wa IsayaYesu—Njia, Kweli, na Uzima
-
-
Inamaanisha nini kwamba “hatagombana wala kupiga kelele, wala yeyote hatasikia sauti yake kwenye barabara kuu”? Yesu anapowaponya watu, hawaruhusu watu hao—au roho waovu—‘wamtangaze.’ (Marko 3:12) Hataki watu wajifunze kumhusu kupitia matangazo ya barabarani yenye kelele au kupitia habari zisizo sahihi ambazo zinapitishwa kwa msisimko kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
-