-
Kesi ya Mahakama ya Ulimwengu Wote Mzima Ambayo Inakuhusisha Wewe NdaniMnara wa Mlinzi—1988 | Februari 1
-
-
21. Ni maswali gani ambayo yanatokezwa na mwito wa ushindani wa Yehova kwa ile miungu ya mataifa?
21 Hivyo, kana kwamba anaambia mahakama, Yehova anasema: “Acheni yale mataifa yote yakusanywe pamoja kwenye mahali pamoja, na acheni vikundi vya kitaifa vikusanywe pamoja... . acheni wao watoe mashahidi wao, kwamba wao wapate kutangazwa waadilifu, au acheni wao wasikie na kusema, ‘Huu ndio ule ukweli!’ “(Isaya 43:9, NW) Huo ni mwito wa ushindani wa moja kwa moja kwa ile miungu ya mataifa. Je! ye yote kati yao anaweza kueleza mambo yaliyo katika wakati ujao? Je! wao waliweza kufanya hivyo katika wakati uliopita? Je! wao wanaweza kupata mmoja ye yote wa kuhimili ushuhuda kwa ithibati madhubuti kwamba miungu hiyo imethibitika kuwa ya kweli, inayostahili ushikaminifu wetu? Ni kumbukumbu gani ambayo ile miungu ya mataifa, na wafuasi wayo, wametokeza katika wakati wetu? Je! imekuwa kumbukumbu nzuri zaidi ya ile ambayo miungu ya Wamisri wa kale, Waashuru, na Wababuloni ilitokeza? Kwa upande ule mwingine, je! wale ambao wanahimili ushuhuda kwa Yehova wametokeza ithibati madhubuti kwamba Yehova ndiye yule Mungu wa kweli, yule Mmoja tu anayestahili ibada yetu? Makala inayofuata itazungumzia mambo hayo.
-
-
Je! Wewe Utakuwa Shahidi kwa Ajili ya Yule Mungu wa Kweli?Mnara wa Mlinzi—1988 | Februari 1
-
-
Mwito wa Ushindani kwa Miungu Mingine
3. Ni mwito wa ushindani gani ambao Yehova anatokeza kwa miungu mingine yote?
3 Yehova alivuvia Isaya pumzi ya kuandika katika kumbukumbu huu mwito wa ushindani kwa miungu mingine yote: “Ni nani aliye miongoni mwao [ile miungu ya mataifa na jamii za watu] ambaye anaweza kueleza jambo hilo [unabii sahihi]? Au je! wao wanaweza kusababisha sisi tusikie hata yale mambo ya kwanza [ambayo yatatukia katika wakati ujao]? Acheni wao [wakiwa miungu] watokeze mashahidi wao, kwamba wao [wakiwa miungu] wapate kutangazwa uadilifu, au acheni wao [zile jamii za watu wa mataifa] wasikie na kusema, ‘Huo ndio ule ukweli!’” (Isaya 43:9, NW) Hivyo Yehova anaitolea mwito wa ushindani miungu yote ambayo watu wanaabudu ithibitishe kwamba hiyo ni miungu. Mashahidi wayo wanapaswa kutokeza ushuhuda kwamba miungu yao inategemeka na inastahili kuabudiwa.
-