-
Yule Mwanamke Tasa AshangiliaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
9, 10. Maagizo ‘kupanua mahali pa hema’ yangemaanisha nini kwa mwanamke aliyeishi hemani nyakati za kale, na kwa nini huo ni wakati wa shangwe kwa mwanamke huyo?
9 Isaya anaendelea kutoa unabii juu ya kipindi fulani cha ukuzi wa kustaajabisha: “Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu. Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.”—Isaya 54:2-4.
10 Hapa Yerusalemu anaambiwa mambo kana kwamba ni mke na mama anayekaa katika mahema, sawa na Sara. Anapobarikiwa kwa kupata familia inayoongezeka, umefika wakati wa mama huyo kuhakikisha kwamba nyumba yake inapanuliwa. Anahitaji kuongeza urefu wa mapazia yake na kamba zake na kuvipigilia imara vigingi vya hema mahali pake papya. Hiyo ni kazi inayomfurahisha, na kwa kuwa huo ni wakati wa shughuli nyingi, anaweza kusahau kwa urahisi miaka mingi aliyoitumia akihangaika bila kujua kama siku moja angezaa watoto wa kuendeleza ukoo wa familia.
-
-
Yule Mwanamke Tasa AshangiliaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
a Kulingana na Ufunuo 12:1-17, “mwanamke” wa Mungu alibarikiwa sana kwa kuzaa ‘mzao’ wa maana sana—si mwana-roho mmoja tu, bali ni Ufalme wa Kimesiya ulio mbinguni. Uzawa huo ulitukia mwaka wa 1914. (Ona Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!, ukurasa wa 177-186.) Unabii wa Isaya unakaza fikira juu ya shangwe ambayo mwanamke huyo anahisi kwa sababu ya baraka ambayo Mungu anawapa wana wake watiwa-mafuta walio duniani.
-