-
Wachungaji Saba Na Watawala Wadogo Wanane Wanatuhusuje Leo?Mnara wa Mlinzi—2013 | Novemba 15
-
-
3 Isaya alisema hivi: “Tazama! Mwanamwali kwa kweli atapata mimba, naye atazaa mwana, naye hakika atamwita jina lake Imanueli. . . . Kabla ya mvulana huyo kujua jinsi ya kukataa lililo baya na kuchagua lililo jema, nchi ya wale wafalme wawili mnaowahofu [Siria na Israeli] na kuchukizwa kwa sababu yao itaachwa kabisa.” (Isa. 7:14, 16) Kwa kweli sehemu ya kwanza ya unabii huo inahusu kuzaliwa kwa Masihi. (Mt. 1:23) Hata hivyo, kwa kuwa ‘wafalme hao wawili,’ yaani, mfalme wa Siria na mfalme wa Israeli hawakuwa tena tishio kwa taifa la Yuda katika karne ya kwanza W.K., bila shaka unabii kuhusu Imanueli ulitimizwa kwa mara ya kwanza katika siku za Isaya.
4 Muda mfupi baada ya Isaya kutoa tangazo hilo muhimu, mke wake alipata mimba na kuzaa mwana aliyeitwa Maher-shalal-hash-bazi. Inawezekana kwamba mwana huyo ndiye “Imanueli” aliyetajwa na Isaya.a Katika nyakati za Biblia, mtoto mchanga alipewa jina moja alipozaliwa. Labda jina hilo liliwakumbusha tukio fulani la pekee, lakini wazazi na watu wake wa ukoo walimpa jina lingine. (2 Sam. 12:24, 25) Hakuna uthibitisho wowote unaoonyesha kwamba Yesu aliitwa Imanueli.—Soma Isaya 7:14; 8:3, 4.
-
-
Wachungaji Saba Na Watawala Wadogo Wanane Wanatuhusuje Leo?Mnara wa Mlinzi—2013 | Novemba 15
-
-
a Neno la Kiebrania linalotafsiriwa “mwanamwali” katika Isaya 7:14 linaweza kumaanisha mwanamke aliyeolewa au bikira. Kwa hiyo, neno hilohilo linaweza kumhusu mke wa Isaya na Maria, bikira Myahudi.
-