-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
25. Ni nini linalotukia juu ya Misri ya kale kwa utimizo wa Isaya 19:1-11?
25 Jirani wa karibu zaidi wa Yuda upande wa kusini ni Misri, adui wa muda mrefu wa watu wa agano wa Mungu. Isaya sura ya 19 yasimulia hali zenye vurugu nchini Misri wakati wa maisha ya Isaya. Kuna vita ya wenyewe kwa wenyewe Misri, kukiwa vita ya “mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.” (Isaya 19:2, 13, 14) Wanahistoria watoa uthibitisho unaohusu nasaba za wafalme zenye kupambana zikitawala sehemu mbalimbali za nchi hiyo kwa wakati mmoja. Hekima wanayojivunia Wamisri, pamoja na ‘sanamu zao, na waganga wao,’ haiwaokoi kutoka katika “mikono ya bwana mgumu.” (Isaya 19:3, 4) Ashuru, Babiloni, Uajemi, Ugiriki, na Roma, zaishinda Misri kabisa. Matukio hayo yote yatimiza unabii mbalimbali wa Isaya 19:1-11.
-
-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
27. Ni migawanyiko ipi ya kindani iliyotabiriwa kuhusu “Misri,” na mambo hayo yanatimizwaje leo?
27 Yehova asema hivi kwa maneno ya unabii kuhusiana na wakati utakaoongoza kwenye kutekelezwa kwa hukumu: “Nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.” (Isaya 19:2) Tangu kusimamishwa kwa Ufalme wa Mungu mwaka wa 1914, “ishara ya kuwapo [kwa Yesu]” imeonekana taifa liinukapo dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Mamilioni ya watu katika siku hizi za mwisho wamekufa kwa sababu ya mauaji ya kikabila, maangamizi ya kijamii yenye umwagikaji wa damu, na maangamizi ya watu wa jamii fulani hususa. “Maumivu [hayo] makali ya ghafula ya taabu” hayana budi kuwa mabaya zaidi mwisho ukaribiapo.—Mathayo 24:3, 7, 8.
-