-
Hukumu ya Yehova Dhidi ya Wafundishaji BandiaMnara wa Mlinzi—1994 | Machi 1
-
-
17. (a) Kulingana na Yeremia, ni hukumu gani ambayo ingelipata Yerusalemu lenye uovu? (b) Ni nini kitakachoipata Jumuiya ya Wakristo hivi karibuni?
17 Wafundishaji bandia wa Jumuiya ya Wakristo watapokea hukumu gani kutoka kwa Yehova, yule Hakimu mkuu? Mistari 19, 20, 39, na 40 yajibu hivi: “Tazama, tufani ya BWANA, [Yehova, NW], yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni dhoruba ya kisulisuli; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani. Hasira ya BWANA, [Yehova, NW] haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake. . . . Nitawasahau ninyi kabisa, nami nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele za uso wangu; nami nitaleta juu yenu aibu ya milele, na fedheha ya daima, ambayo haitasahauliwa.” Yote hayo yalipata Yerusalemu lenye uovu na hekalu lalo, na sasa msiba kama huo utaipata Jumuiya ya Wakristo yenye uovu hivi karibuni!
-
-
Hukumu ya Yehova Dhidi ya Wafundishaji BandiaMnara wa Mlinzi—1994 | Machi 1
-
-
21. (a) Kwa nini Yerusalemu liliharibiwa katika 607 K.W.K.? (b) Baada ya Yerusalemu kuharibiwa, ni nini kilichowapata manabii bandia na kumpata nabii wa kweli wa Yehova, hilo likitupa sisi uhakikishio gani leo?
21 Yehova ilitekelezwa katika siku ya Yeremia Wababiloni walipoharibu Yerusalemu katika 607 K.W.K. Kama ilivyotolewa unabii, hiyo ilikuwa ‘aibu na fedheha’ kwa Waisraeli hao wakaidi, wasio waaminifu. (Yeremia 23:39, 40) Liliwaonyesha kwamba Yehova, ambaye walikuwa wamekosa kumheshimu mara kwa mara, hatimaye alikuwa amewaacha wapatwe na matokeo ya ubaya wao. Hatimaye vinywa vya manabii wao bandia wenye kiburi vilinyamazishwa. Lakini, kinywa cha Yeremia kiliendelea kutoa unabii. Yehova hakumwacha. Kupatana na kiolezo hicho, Yehova hataacha jamii ya Yeremia wakati hukumu yake nzito iongozapo kwenye kuponda na kuwaangamiza makasisi wa Jumuiya ya Wakristo na wale wanaoamini uongo wao.
-