MWANAMKE ALIYE HURU
Mwanamke ambaye hayuko utumwani. Usemi huu hutumiwa kumrejelea Sara, mke wa Abrahamu, na “Yerusalemu la juu.” Kuanzia kipindi ambapo Yehova Mungu alipowaweka huru Waisraeli kutoka katika utumwa wa Wamisri na akawapa Sheria katika Mlima Sinai mpaka agano la Sheria lilipokomeshwa mwaka wa 33 W.K., Yehova alilitendea taifa la Israeli kama mke wa pili. (Yer 3:14; 31:31, 32) Hata hivyo, Sheria haikulipatia taifa la Israeli hadhi ya kuwa mwanamke huru kwa sababu iliwaonyesha Waisraeli wakiwa chini ya dhambi, hivyo walikuwa watumwa. Ndio sababu Paulo alilinganisha Yerusalemu lililokuwa mtumwa katika siku zake na Hagari, kijakazi wa Abrahamu, na “watoto,” au raia wa Yerusalemu, na Ishmaeli, mwana wa Hagari. Kinyume na hilo, mke wa asili wa Mungu, Yerusalemu la juu, sikuzote amekuwa mwanamke aliye huru kama Sara na watoto wake vilevile. Ili kuwa mtoto huru wa Yerusalemu la juu, ukiwa na “uhuru” kama wake, ni muhimu kuwekwa huru na Mwana wa Mungu kutoka kwenye utumwa wa dhambi.—Gal 4:22–5:1; Yoh 8:34-36.