-
Ni Nini Kusudi la Mungu kwa Ainabinadamu?Je! Ulimwengu Usio na Vita Utakuwako Wakati Wowote?
-
-
20, 21. (a) Ni nini kinachoahidiwa kwenye Yeremia 31:31-34? (b) Kusudi lililotaarifiwa la agano jipya lilikuwa nini? (c) Likiwa tokeo, kungetukia nini kwa agano la Sheria?
20 Ilikuwa yapata miaka 900 baada ya Musa kwamba Yeremia aliwasilisha kwa taifa la Israeli maneno ya Mungu: “Ona, wakati waja—ajulisha BWANA—ambapo mimi nitafanya agano jipya na Nyumba ya Israeli na Nyumba ya Yuda. Halitakuwa kama lile agano ambalo nilifanya pamoja na baba zao, wakati mimi nilipowachukua kwa mkono kuwaongoza kutoka nchi ya Misri, agano ambalo walivunja, . . .—ajulisha BWANA. Bali ndivyo lilivyo agano nitakalofanya pamoja na Nyumba ya Israeli baada ya siku hizi . . . Mimi nitasamehe maovu yao, na nisikumbuke dhambi zao tena.”d—Yeremia 31:31-34.
21 Ikiwa nabii kama Musa atumika akiwa mpatanishi mpya wa agano jipya, basi inakuwa wazi pia kwamba yale mambo mengi madogomadogo hususa ya ibada yaliyotakwa chini ya Sheria ya Musa yasingetumika daima ila tu mpaka lile agano jipya lisimamishwe. Hakika, wakati Mungu angeandaa msingi wa ‘kusamehe maovu yao na asikumbuke dhambi zao tena,’ kusingekuwa tena na uhitaji wa mfumo mzima wa dhabihu ulioandaliwa na mpango wa hekalu, ulioleta msamaha wa kitambo tu. Kwa kuanzishwa kwa agano jipya, pande za kisherehe za agano la Sheria, kama vile kushika Sabato na sikukuu mbalimbali, pia kusingekuwa na maana ileile. Kwa wakati wake, hakika Mungu angefunua ni nini lingetakwa kwa wale walio katika mpango huo wa agano jipya lililoahidiwa.—Amosi 3:7.
-
-
Ni Nini Kusudi la Mungu kwa Ainabinadamu?Je! Ulimwengu Usio na Vita Utakuwako Wakati Wowote?
-
-
d Ufafanuzi uliokubaliwa wa Dini ya Kiyahudi ya ki-siku-hizi ni kwamba Yeremia alikuwa akitabiri tu kufanywa upya na kuthibitishwa upya kwa agano la Sheria pamoja na Israeli, kama ilivyotukia baada ya kurudi kwao kutoka uhamisho katika Babuloni katika 537 K.W.K. (Ezra 10:1-14) Lakini kwa mara nyingine tena unabii wenyewe hukanusha ufafanuzi kama huo. Mungu alitaarifu waziwazi kwamba hilo litakuwa “agano jipya,” si agano lililofanywa upya tu. Zaidi ya hilo, yeye akazia kwamba si kama lile agano lililofanywa wakati alipowaongoza kutoka katika utumwa wa Misri. Baadhi yao wamesema kwamba lilikuwa “jipya” katika maana ya kwamba sasa wangelishika kwa uaminifu agano lilo hilo, lakini historia huonyesha tofauti. Kwa kweli, ukosefu wao wa uaminifu uliongoza kwenye uharibifu wa lile hekalu la pili.—Kumbukumbu la Torati 18:19; 28:45-48.
-