-
Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia?Amkeni!—2007 | Novemba
-
-
Mnamo 2005, wataalamu wa vitu vya kale walipokuwa wakichimbua eneo ambapo walitarajia kupata jumba la Mfalme Daudi, walipata jengo kubwa la mawe ambalo walifikiri liliharibiwa Wababiloni walipoteketeza Yerusalemu zaidi ya miaka 2,600 iliyopita, katika siku za nabii wa Mungu Yeremia. Hakuna uhakika kwamba jengo hilo ni mabaki ya jumba la Mfalme Daudi. Hata hivyo, mtaalamu wa vitu vya kale Eliat Mazar aligundua kitu kimoja chenye kupendeza chenye upana wa sentimita 1, yaani, muhuri wa udongo [5] wenye maandishi yaliyosema: “Wa Yehukali mwana wa Shelemiyahu mwana wa Shovi.” Yaonekana hayo ni maandishi ya muhuri wa Yehukali (pia Yukali), ofisa Myahudi anayetajwa katika Biblia ambaye alikuwa mpinzani wa Yeremia.—Yeremia 37:3; 38:1-6.
Mazar anasema kwamba Yehukali ndiye “waziri wa pili wa mfalme,” baada ya Gemaria, mwana wa Shafani, ambaye jina lake liko kwenye muhuri uliopatikana katika Jiji la Daudi. Biblia inamtambulisha Yehukali, mwana wa Shelemia (Shelemiyahu), kuwa mkuu wa Yuda. Kabla ya ugunduzi huo, hakutajwa mahali pengine popote nje ya Maandiko.
-
-
Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia?Amkeni!—2007 | Novemba
-
-
3: Musée du Louvre, Paris; 4: Photograph taken by courtesy of the British Museum; 5: Gabi Laron/Institute of Archaeology/Hebrew University © Eilat Mazar
-