-
“Nitamweka Mchungaji Mmoja”Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
-
-
5. Fumbo hilo linahusisha nini?
5 Soma Ezekieli 17:3-10. Ufuatao ni muhtasari wa fumbo hilo: “Tai mkubwa” anachukua chipukizi lililo juu zaidi la mwerezi na kuliweka katika “jiji la wafanyabiashara.” Kisha tai huyo anachukua “baadhi ya mbegu za nchi hiyo” na kuzipanda katika shamba lenye rutuba “kando ya maji mengi.” Mbegu hiyo inasitawi na kuwa ‘mzabibu unaotambaa.’ Kisha “tai mwingine mkubwa” anatokea. Mizizi ya ule mzabibu inasambaa “kwa bidii kuelekea” yule tai wa pili ikitaka kupandwa tena katika eneo lingine lenye maji. Yehova anashutumu matendo ya mzabibu huo, na kuonyesha kwamba mizizi yake itang’olewa nao ‘utakauka kabisa.’
6. Fafanua maana ya fumbo hilo.
6 Fumbo hilo lilimaanisha nini? (Soma Ezekieli 17:11-15.) Mwaka wa 617 K.W.K., Mfalme Nebukadneza wa Babiloni (“tai mkubwa” wa kwanza) alizingira Yerusalemu. Alimchukua Mfalme Yehoyakini wa Yuda (“chipukizi lililo juu zaidi”) kutoka kwenye kiti chake cha Ufalme na kumpeleka Babiloni (“jiji la wafanyabiashara”). Nebukadneza alimweka Sedekia (mmoja wa “mbegu za nchi” wa familia ya kifalme) awe mtawala huko Yerusalemu. Mfalme mpya wa Yuda aliapishwa katika jina la Mungu, na hivyo kuwajibika kuwa mshikamanifu akiwa mfalme kibaraka. (2 Nya. 36:13) Lakini Sedekia alipuuza kiapo chake; akaasi dhidi ya Babiloni na kugeukia Farao wa Misri (yule “tai mkubwa” wa pili) ili kupata msaada wa kijeshi lakini hakufanikiwa. Yehova alishutumu matendo yasiyo ya uaminifu ya Sedekia aliyevunja kiapo. (Eze. 17:16-21) Mwishowe, Sedekia aling’olewa mamlakani, na kufa gerezani huko Babiloni.—Yer. 52:6-11.
-
-
Unabii Kumhusu Masihi—Mwerezi MkubwaHatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
-
-
2. Nebukadneza amweka Sedekia kuwa mtawala huko Yerusalemu
-