-
Danieli Kitabu Kilichohakikishwa Kuwa cha UnabiiMnara wa Mlinzi—1986 | Oktoba 1
-
-
Danieli alisimulia hivi: “Naliona katika maono yangu wakati wa usiku . . . Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama simba . . . Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu . . . Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui . . . Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi . . . Wanyama hawa wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani. Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.”—Danieli 7:2-18.
-
-
Danieli Kitabu Kilichohakikishwa Kuwa cha UnabiiMnara wa Mlinzi—1986 | Oktoba 1
-
-
Vivyo hivyo, wale wanyama wanne wa Danieli sura ya 7 wanafananisha serikali kubwa nne za ulimwengu zinazoanzia siku za Danieli na kuendelea, mpaka wakati wa kusimamishwa kwa Ufalme wa Mungu. Danieli aliishi hata baada ya anguko la Serikali Kubwa ya Ulimwengu ya Babuloni (yule simba) na mpaka mwanzo wa serikali iliyofuata hiyo, Muungano wa Umedi na Uajemi (yule dubu). Unabii wa Danieli ambao ungetukia baada ya muda mrefu ulitabiri anguko la Muungano wa Umedi na Uajemi mbele ya Ugiriki (Uyunani, yule chui), ambao nao ungeondolewa hata mahali pao pachukuliwe na “mnyama wa nne,” ile Milki ya Kiroma na chipukizi iliyotokana nao, Serikali Kubwa ya Ulimwengu ya Muungano wa Waingereza na Waamerika.b
-