-
Kifo cha TaifaMnara wa Mlinzi—1989 | Aprili 1
-
-
Mhofu Yehova, si wapinzani. Uharibifu wa Israeli ungeweza kuletwa na bumba la nzige au moto wenye kula vitu vyote. Amosi alisihi Mungu kwa niaba ya Israeli, na “Bwana [Yehova, NW] akaghairi” kuhusu hukumu yake, hivi kwamba haikutekelezwa hivyo. Hata hivyo, kama mjenzi achunguzaye uwima wa ukuta kwa kutumia timazi, Yehova ‘hatawapita tena kamwe’ Israeli (‘hatawaachilia tena zaidi ya hapo, NW). (Amosi 7:1-8) Ni lazima taifa hilo lifanywe ukiwa. Kwa kukasirishwa sana na ujumbe wa mnabii huyo, Amazia, kuhani wa ibada ya ndama, anamshtaki Amosi kwa ubandia juu ya kumfitini mfalme na kumwagiza ‘aikimbilie nchi ya Yuda asitabiri tena’ Betheli. (Amosi 7:12, 13) Je! Amosi anajikunyata kwa woga? Sivyo! Bila hofu anatabiri kifo cha Amazia na afa kwa jamaa yake. Kama vile matunda hukusanywa wakati wa mavuno, ndivyo ulivyo wakati wa Yehova kufanya hesabu pamoja na Israeli. Hakutakuwako kuponyoka.—Amosi 7:1-8:14.
-
-
Kifo cha TaifaMnara wa Mlinzi—1989 | Aprili 1
-
-
○ 7:1—‘Mimea ya baada ya mavuno ya mfalme’ inaelekea zaidi kuwa ilimaanisha kodi au malipo ya heshima za kujinyenyekeza ambazo mfalme alitoza ili kuwaandalia chakula wanyama wake na askari wapanda-farasi. Kodi ya mfalme ilipasa kulipwa kwanza, kisha watu wangeweza kuipata “mimea” (nyasi, NW), au majani, kwa matumizi yao wenyewe. Lakini kabla hawajaweza kufanya hivyo, nzige wakaja na kuyala yote hayo yaliyopandwa baadaye.
-