-
Alijifunza Kutokana na Makosa YakeIgeni Imani Yao
-
-
12. (a) Kwa nini hatupaswi kumhukumu Yona haraka kwa sababu ya kulala huku dhoruba ikipiga? (Ona pia maelezo ya chini.) (b) Yehova alifunuaje chanzo cha matatizo?
12 Huku akihisi hawezi kusaidia, Yona alienda chini kwenye sehemu za ndani kabisa za meli hiyo na akapata mahali pa kupumzikia. Akalala fofofo.b Kapteni alimpata Yona, akamwamsha, na kumhimiza amwombe mungu wake, kama kila mtu alivyokuwa akifanya. Wakiwa na hakika kwamba haikuwa dhoruba ya kawaida, mabaharia walipiga kura ili kuona ni nani aliyekuwa amewaingiza mashakani. Yona alizidi kuwa na wasiwasi kadiri walivyoendelea kupiga kura. Baada ya muda ukweli ukaonekana. Yehova alikuwa akielekeza dhoruba, kutia ndani kura imwangukie mtu mmoja—Yona!—Soma Yona 1:5-7.
-
-
Alijifunza Kutokana na Makosa YakeIgeni Imani Yao
-
-
b Tafsiri ya Septuajinti inakazia jinsi Yona alivyolala fofofo kwa kuongezea kwamba alikuwa akikoroma. Hata hivyo, badala ya kuona usingizi wa Yona kama ishara ya kutojali, tunapaswa kukumbuka kwamba nyakati fulani watu walioshuka moyo hupatwa na usingizi. Yesu alipokuwa na uchungu mwingi katika bustani ya Gethsemane, Petro, Yakobo, na Yohana walikuwa “wakisinzia kwa huzuni.”—Luka 22:45.
-