-
Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
-
-
17. Kulingana na Sefania 1:14-16, siku ya hukumu ya Yehova i karibu kadiri gani?
17 Siku ya hukumu ya Yehova i karibu kadiri gani? Kulingana na Sefania 1:14-16, Mungu ahakikisha hivi: “Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; i karibu, nayo inafanya haraka sana; naam, sauti ya siku ya BWANA; shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko! Siku ile ni siku ya ghadhabu, siku ya fadhaa na dhiki, siku ya uharibifu na ukiwa, siku ya giza na utusitusi, siku ya mawingu na giza kuu, siku ya tarumbeta na ya kamsa, juu ya miji yenye maboma, juu ya buruji zilizo ndefu sana.”
-
-
Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
-
-
19, 20. (a) Ni baadhi ya mambo gani yaliyohusika katika kudhihirishwa kwa hasira ya kisasi ya Mungu dhidi ya Yuda na Yerusalemu? (b) Kwa kuzingatia uharibifu utakaowapata watu waovu wa mfumo huu wa mambo, ni maswali gani yanayozuka?
19 Ilikuwa “siku ya fadhaa na dhiki” wakati Mungu alipodhihirisha ghadhabu yake dhidi ya Yuda na Yerusalemu. Wavamizi wa Babiloni walisababisha mateso mengi kwa wakazi wa Yuda, pamoja na maumivu makali ya akili, wakati walipokabili kifo na uharibifu. “Siku hiyo ya uharibifu na ukiwa” ilikuwa siku ya giza, mawingu, na utusitusi, huenda si katika njia ya ufananisho tu bali pia kihalisi kwa kuwa moshi na mauaji yalikuwa kila mahali. Ilikuwa “siku ya tarumbeta na ya kamsa,” lakini maonyo yalitolewa bure.
20 Walinzi wa Yerusalemu walikuwa hoi wakati magogo ya Babiloni yalipovunja “buruji zilizo ndefu sana.” Ngome za mfumo huu mwovu wa mambo zitakuwa bure dhidi ya silaha za vita alizo nazo Mungu mbinguni, ambazo ziko tayari kutumiwa naye hivi karibuni anapoharibu watu waovu. Je, unatumaini kuhifadhiwa? Je, umechukua msimamo imara upande wa Yehova, ‘ambaye huwahifadhi wote wampendao, na kuwaangamiza wote wasio haki’?—Zaburi 145:20.
-