Tamasha za Kutoka Lile Bara la Ahadi
Mataifa Yakusanyika Megido
“WATAFITI ni vigeugeu kuhusiana na Har-Magedoni ya ulimwengu,” ikaripoti makala moja ya kisayansi juu ya kama vita ya nyukilia ingeleta “kipupwe cha nyukilia” chenye barafu ya kugandisha, au ingeleta “kiangazi cha nyukilia.”
Labda wewe umeona maelezo ya jinsi hiyo yenye kuhusianisha “Har-Magedoni” na nyakati zetu za hatari. “Har-Magedoni” ni nini? Huenda wewe ukataka kujua, kwa kuwa uhai wako unahusika.
Tazama juu kwenye mandhari ya Megido yenye kuonekana kutoka angani. Eneo hili katika Israeli ya kale lilifaa sana kwa utumizi wa mbinu nyingi. Mtume Yohana alitumia jina la eneo hilo alipoandika juu ya “mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni [Mlima wa Megido],” au Armagedoni. (Ufunuo 16:16) Kujua mandhari-nyuma ya Megido kunamulikia mwanga maneno hayo.
Unaweza kuona mahali eneo hilo lilipokuwa katika ramani iliyoambatanishwa. Mahali hapo ni kama palitazamana na barabara mbili kuu. Milima ya Karmeli ilitilia kipingamizi ile njia ya kutoka Kaskazini kwenda Kusini, iliyo kati ya Misri upande wa kusini na Dameski au majiji mengine kuelekea Eufrati upande wa kaskazini. Kwa hiyo majeshi na misafara yenye kufanya biashara ililazimishwa kupitia kipitio cha kimo cha chini kando ya Megido, kipitio kile kilicho upande wa kulia wa picha. Katika Bonde la Yezreeli, barabara iliyopitia eneo hilo kutoka Kaskazini kwenda Kusini ilikatizana na njia ile mashuhuri kati ya Tiro na Bonde la Yordani, au Samaria na Yerusalemu. Kwa kukaa likiwa limetagaa kwenye njia hizo, eneo la Megido lingeweza kuwa ni kama limewatawala kabisa wenye kupitia humo, na bonde lililokuwa mbele ya Megido lilikuja kuwa mahali pa mapigano ya kukata maneno.
Mathalani, hapo ndipo Hakimu Baraka aliposhinda Wakanaani wakiwa chini ya Sisera mkuu wa jeshi, aliyekuwa na magari-vita 900 yenye miundu ya chuma. (Waamuzi 4:1-3,12-16; 5:19) Baadaye, Farao Neko aliongoza kani ya Kimisri yenye nguvu nyingi ya askari na magari-vita kukwea njia ile ya pwani (kwa sababu hiyo ikawa na jina Via Maris, au Njia ya Bahari) ili kuwaongezea kani Waashuri karibu na Eufrati. Kwa sababu fulani, Yosia mfalme Myudea aliamua kufanya pambano la kimataifa pamoja na Neko. Lakini mahali gani? Yosia alichagua uwanda ulio karibu na Megido, ingawa ulikuwa kama kilometa 90 kuelekea kaskazini mwa Yerusalemu.—2 Mambo ya Nyakati 35:20-22; Yeremia 46:2.
Yeye alijua kwamba ilikuwa lazima Wamisri wapitie pale, na huenda ikawa alihisi kwamba yeye ndiye angepata faida zaidi, kwa maana angekuwa karibu na ngome ya Kiisraeli. Kama vile unavyoweza kuona, Tell (tungamo la ardhi la) Megido ni kubwa sana. Jiji hilo la kale halingeweza kushindwa kwa urahisi. Sulemani aliimarisha Megido, kwa uwazi akijenga kuta za mawe zilizotungamana sana, na lango kubwa sana la kulihami.a (1 Wafalme 9:15) Upande wa kushoto wa hilo tungamo la ardhi, unaweza kuona shimo kubwa lenye umbo mstatili, lililokuwa mwingilio wa mfumo tata wa ugavi-maji. Vidato vilivyoinama sana viliongoza chini kwenye mtaro mrefu uliopasuliwa kupitia mwamba wa chinichini, hiyo ikiwapa Waisraeli njia ya kufikia jicho la maji hali wakiwa wamehamiwa wasishambuliwe. Wachimbuzi wa vitu vya kale wamegundua pia mabakio ya banda la farasi kama 450, labda yakiwa ni ya kutoka wakati wa utawala wa Ahabu.—Linganisha 1 Wafalme 9:19.
Katika pigano hilo la kukata maneno karibu na Megido, Yosia alipata jeraha la kifo, akafa akiwa njiani kurudi Yerusalemu. (2 Wafalme 23:28-30) Huenda ikawa hiyo ndiyo ilisababisha yale ‘maombolezo [kupiga mayowe, NW] katika bonde la Megido’ ambayo yanatajwa kwenye Zekaria 12:11. Si muda mrefu baada ya ushinde wa Yosia, Babuloni ilieneza uvutano wayo wa kijeshi ukaingia katika Yudea iliyodhoofishwa.—2 Wafalme 24:1, 2, 12-14; 2 Mambo ya Nyakati 36:1-6.
Ukiwa na habari hizo za mandhari-nyuma, unaweza kuthamini ni kwa nini katika Ufunuo aliopewa mtume Yohana, eneo la Megido lingeweza kutumiwa katika kutabiri mkusanyo wa “‘wafalme wa ulimwengu wote” kwenye “vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.” Hakuna kisehemu chochote kimoja duniani, na kwa uhakika si ule uwanda-bonde wenye kumilikiwa na Tell Megido, ambacho kingeweza kutia ndani mataifa yote yenye kupinga Mungu. Lakini Har-Magedoni, au Armagedoni, kwa kufaa huwakilisha kituo cha hali ya vita hiyo ya kukata maneno.—Ufunuo 16:14, 16; 19:11-21.
Kwa hiyo acha wanasiasa na watangaza-habari wafikiri kimakosa kwamba Armagedoni ni vita ya nyukilia ambayo ingeteketeza tufe letu. Kwa kufikiria historia ya Megido, unaweza kuelewa jambo hilo kwa usahihi zaidi. Unaweza kuthamini kwamba Har-Magedoni ni kituo cha hali ambamo muda si muda mataifa yataletwa kwa ajili ya ile vita kuu wakati ambapo Mungu atafutilia mbali mfumo mbovu wa sasa, hiyo ikifungulia njia ulimwengu mpya ulio mwadilifu.—2 Petro 3:11-13.
[Maelezo ya Chini]
a Unaweza kusoma katika Mnara wa Mlinzi wa Agosti 15, 1988, kurasa 24-6, usimulizi wa kusisimua juu ya lango la Megido.
[Ramani katika ukurasa wa 17]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Great Sea
To Damascus
To Tyre
Sea of Galilee
Acco
Caramel Range
Megiddo
Via Maris
Joppa
To Egypt
Beth-Shean
Dothan
Samaria
Shechem
To Jerusalem
Jordan River
Mi 0 10
Km 0 10 20
[Credit Line]
Msingi wake ni ramani ambayo haki za kuinakili zimechukuliwa na Pictorial Archive (Near Eastern History) Est and Survey of Israel
[Picha katika ukurasa wa 16]
UTAPATA mandhari kubwa zaidi ya Megido katika 1989 Calendar of Jehouah’s Witnesses. Picha zayo sita zitazungumziwa mwaka huu katika makala za Mnara wa Mlinzi, ambazo ukitaka unaweza kuziweka pamoja na kalenda yenyewe kwa utumizi wa wakati ujao.
[Credit Line]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.
[Picha katika ukurasa wa 17]
MCHONGO huu wa Kimisri unaweza kukusaidia uone akilini mwako Farao Neko akisonga mbele kupita Megido, ambako alimshindia Mfalme Yosia
[Credit Line]
Pictorial Archive (Near Eastern Historv) Est.